HUYU NDIYO MREMBO MWENYE ULEMAVU WA NGOZI AANAYEDAIWA KUHUKUMIWA ZAIDI YA MARA TANO KWA KOSA LA KUUZA MWILI.


Emmily Omari akiwa selo.

 MREMBO mwenye ulemavu wa ngozi, Emmily Omari, 23, mkazi Buguruni, Dar anayedaiwa kujihusisha na biashara haramu ya uchangudoa, hivi karibuni alipandishwa kizimbani kwa madai ya kufanya kosa hilo.

Emmily ambaye amekuwa akiwatesa askari polisi ambao wamekuwa wakimkamata mara kwa mara na kumfikisha mahakamani lakini haachi tabia hiyo, alipandishwa katika Mahakama ya Jiji na kusomewa mashtaka yake.

Hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo, Timothy Lyon alipigwa butwaa kumuona mrembo huyo ambaye aliwahi kumhukumu zaidi ya mara tano kwa kosa la kujiuza na kumuachia huru baada ya kulipa faini.NA VITUKO VYA MTAA

Pilato huyo baada ya kumuona tena Emmily mbele yake akikabiliwa na shitaka lilelile, alimuuliza alikuwa na tatizo gani lililosababisha mara kwa mara afikishwe mahakamani hapo, mrembo huyo hakujibu chochote. 
“We Emmily sasa unatuletea utani, kila siku unaletwa hapa tunakupiga faini unalipa unatoka na kwenda kurudia hiyo biashara yako… sasa tunaona kama unatufanyia masihara  sasa leo hakuna cha faini wala dhamana uende Segerea ukale dona la bure labda utajifunza,” alisema Hakimu Lyon na kuwaamuru askari wampandishe kwenye Karandinga kwa ajili ya safari ya gerezani.

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana juzikati zinaeleza kuwa mrembo huyo baada ya kukaa Segerea kwa wiki mbili, alipewa dhamana wakati mahakama ikiendelea kumjadili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA