JICHO LA SUFIANIMAFOTO KUTOKA ABUJA NIGERIA, VICHWA VYA MBUZI KAMA NJUGU

 Kijana mfanyabiashara akipita katika mitaa ya Jiji la Abuja, akiwa na Sinia lenye Vichwa vya Mbuzi akitafuta wateja. haikuweza kufahamika kuwa Mbuzi hao walichinjwa muda gani na kama kuna uwezekano wa Kijana huyo kumaliza Vichwa vyote kwa siku, na iwapo vikibaki anatumia utaratibu gani kuvihifadhi hadi kuviuza tena siku inayofuata.
 Mfanyabiashara wa Maziwa akiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abuja, akiwa na chupa anayotumia kupima na kuuzia maziwa hapa akisubiri wateja ambao wengi wao ni wasafiri wanaoshuka katika ndege zinazotua katika uwanja huo.
 Miundombinu na ujenzi wa Barabara si katika Jiji la Dar tu hadi Abuja bado wanaendelea na ujenzi, lakini wao tayari wanamafly over kibao.
 Hata foleni ni kama Dar lakini ni kutokana na ujenzi.
 Hata wafanyabiashara wadogo wadogo wa barabarani Machinga ni kama Dar, hapa wakipita katikati ya magari kunadi biashara zao.
 Lakini katika Jiji la Abuja, asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa vitu vya mkononi kama matunda, mboga na vinginevyo ni wachichana wadogo wadogo kuliko vijana wa kiume.
 Kama unavyoona hapa wakisubiri wateja na mmoja akimkimbilia mteja wake katika moja ya gari...
 Msichana mmoja akimuuzia mteja wake biashara yake hapa akipokea pesa yake.
 Huyu ndiyo kijana pekee aliyeweza kuonekana anga hizi akiwa na Mayai..
 Askari wa Jeshi la Abuja akiongoza magari katika eneo hilo kuyaongoza katika barabara moja kutokana na ujenzi wa barabara hiyo unaoendelea.
Huku ni tofauti na Dar, ambapo wengi tumezoea kwenda kupata huduma ya kuchenji pesa za kigeni katika maduka ya kuchenjia fedha hizo, Hawa ni baadhi tu ya wazee wa Jiji la Abuja, wakiwa wamepozi wakisubiri wateja ili kuwachenjia fedha. Wazee hawa kila mmoja anatembea na pesa zake katika mfuko ambapo kila mteja anayefika humalizana hapa hapa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI