KICHANGA CHAZALIWA NA TASBIHI SHINGONI NCHINI NIGERIA.

Mtoto wa kike aliyezaliwa akiwa amevaa Tasbihi shingoni.

WAKATI leo Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan tisa , kumeibuka maajabu, mtoto wa kike amezaliwa akiwa amevaa Tasbihi shingoni.

Tukio hilo lilijiri katika hospitali binafsi ya uzazi kwenye Jiji la Kotaworo, eneo la Bida, jimboni Niger State nchini Nigeria, Jumapili iliyopita ambapo maelfu ya watu walikusanyika kwa lengo kumshuhudia mtoto huyo.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Naija, mama wa mtoto huyo, Adijat alikimbizwa hospitali karibu na nyumbani kwa Alhaji Mohammed Bello Masaba, majira ya saa 8:00 mchana na baada ya pilika za uzazi, alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.

Mmiliki wa hospitali hiyo ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi hilo la kujifungua alisema: “Nilishtuka nilipoona mtoto anatoka akiwa na Tasbihi nyeusi shingoni.

“Nilishangaa baada ya muda Tasbihi hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe.”

Mara baada ya habari hiyo kusambaa, maelfu ya watu walifika hospitalini hapo wakisema: “Allahu Akibar…Allahu Akibar (Mungu mkubwa…Mungu mkubwa).

Baada ya taarifa hiyo ya ajabu kusambaa watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchini Nigeria walifurika kumwona mtoto huyo wengine wakimgusa.

Juhudi za kumpata baba wa mtoto huyo aitwaye Isah zilishindikana.

You might also like:

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA