MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA WATANZANIA WAISHIO ABUJA NIGERIA, AONDOKA LEO KUREJEA TANZANIA
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
baadhi ya Watanzani ya waishio mjini Abuja, wakati alipokutana nao katika Makazi
ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Nigeria, jana Julai 16, 2013 na kufanya nao
mazungumzo. Makamu ameondoka leo mjini Abuja kurejea nchini Tanzania, baada ya
kuhudhuria Mkutano wa 12 wa siku mbili wa Afrika uliokuwa ukijadili magonjwa ya
Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt.
Goodluck Jonathan, Julai 15-16, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na
Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Kushoto kwake ni mkewe, Mama Asha
Bilal.
Kaimu Balozi wa
Tanzania nchini Nigeria, aliyemaliza muda wake, Siwajibu Baraka Siwajibu,
akiwatambulisha baadhi ya Watanzania kwa makamu wa Rais, wakati alipofika
kuzungumza nao katika Makazi ya Balozi wa Tanzania, Abuja Nigeria jana Julai 16,
2013. Kushoto ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal, na kutoka (Kulia) ni
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi na Kaimu Balozi wa Tanzania
nchini Nigeria, Fatma Rajabu.
Baadhi ya
watanzania waishio Abuja, wakimsikiliza Makamu, Dkt. Bilal, (hayupo pichani)
wakati akizungumza nao.
Baadhi ya
watanzania waishio Abuja, wakimsikiliza Makamu, Dkt. Bilal, (hayupo pichani)
wakati akizungumza nao.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha
Bilal, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Fatma Rajabu na Kaimu Balozi wa
Tanzania, nchini Nigeria, aliyemaliza muda wake, Siwajibu Baraka Siwajibu,
wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya watanzania waishio
Abuja, baada ya makamu kufanya nao mazungumzo
jana.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha
Bilal, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Fatma Rajabu, wakiwa katika
picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya watanzania waishio Abuja, baada ya
makamu kufanya nao mazungumzo jana.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha
Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya watanzania
waishio Abuja, baada ya makamu kufanya nao mazungumzo
jana.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
Mzee,Salu Salatu, ambaye ni raia wa Nigeria aliyefanya kazi katika Ubalozi wa
Tanzania nchini Nigeria kwa muda wa Miaka 25 hadi sasa, baada ya Makamu
kuzungumza na Watanzania waishio Abuja jana Julai 16, 2013. Makamu ameondoka leo
mjini Abuja kurejea Tanzania baada ya kuhudhuria Mkutano wa 12 wa siku mbili wa
Afrika uliokuwa ukijadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12)
uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, Julai 15-16, 2013 mjini
Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za
Afrika.
Comments