MADHAHABU YASICHAFULIWE

Na John Banda,Dodoma.

VIONGOZI wa Madhehebu ya Dini Nchini wametakiwa kukataa kutumiwa kama mameneja kampeni wa wanasiasa wanaotaka madaraka ya uongozi wa taifa.
 
Ushauli huo umetolewa  na Katibu Mkuu  wa Umoja wa madhehebu ya Kikristo Mkoa wa Dodoma Askofu Dk. Elia Mauza alipokuwa akitoa mada kuhusu kuimarishana katika utambuzi wa viashiria vya kuondoa amani katika taifa.
 
Askofu huyo alisema hivi sasa kuna kila dalili zinazoonyesha kuondoka kwa amani na utulivu uliopo hapa nchini na kama havitadhibitiwa kuna hatari ya amani hiyo kutoweka.
 
Mauza alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa  kuwatumia viongozi wa madhehebu ya dini katika kujipatia uongozi ndani na nje ya nchi.
 
Alisema wao kama viongozi wa dini wanatakiwa kutekeleza maagizo ya Mungu na siyo matakwa ya mtu au kikundi cha watu wachache wanotaka madaraka kupitia dini.
 
Katibu huyo alisema jambo hilo ni hatari kwa amni ya nchi kwa viongozi hao wa dini kuwa mameneja wa kampeni za wataka uongzi hao.
 
“Tukitaka kudumu katika nafasi aliyotupa mwenyezi Mungu  au kuendelea kuwa na heshima hiyo ni lazma kujiepusha kutumiwa na watu wa aina hiyo” alisema mauza.
 
Alisema katika kipindi cha nyuma Mitume na manbii waliweza  kutumia nafasi zao vyema  kwani hawakukubali kutumiwa na viongozi ila wao walitoa maelekezo kwa viongozi yaliyotoka kwa Mungu.
 
“kazi yetu kama viongozi wa Dini ni kuwaoombea na kuwashauri lakini tukijiingiza ndani ya kampeni tutakuwa ni watuhumiwa” alisistiza.
 
Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustafa Rajab alisema baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa mwanya kutumika kwa madhabau kama majukwaa ya kisasa.
 
Alisema si sahihi kuruhusu wanasiasa kutumia madhabahu kuhubiri siasa na chuki ingawa anatoa msaada  lakini watu hao wanakuwa na maslahi yao ya kisiasa kupitia madhabau hayo.
 
“wanafika katika maeneo yetu tunawapa nafasi wazungumze lakini badala yake wanahubiri siasa na hata mara nyingine kujenga chuki miongoni mwa dini au vyama vya siasa”” alisema
 
Alisema ni vyema ukajengwa ukuta kati ya viongizi wa dini na wanasiasa ili kila mmoja wao afanye kazi yake badala ya kutumia dini kama daraja la kujipatia uongozi.
 
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.