Mama Obama ampongeza Mama Kikwete kwa kazi anayoifanya ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama pamoja na Mama Laura Bush, mke wa Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush kwenye hoteli ya Serena tarehe 2.7.2013.
 *************************
Na Anna Nkinda - Maelezo

Mke  wa Rais  wa Marekani  Mama  Michelle Obama amempongeza  Mke wa Rais  Mama  Salma  Kikwete  kwa kazi  kubwa anayoifanya  ya kutoa elimu bure  kwa watoto Wa kike ambao ni yatima  na wanaoishi katika mazingira hatarishi .

Mama Obama  alizitoa pongezi hizo leo wakati wa majadiliano baina yake na Mama Laura Bush kwenye mkutano wa   wake Wa Marais Wa afrika unafanyia katika hoteli ya Serena  jijini Dar es  Salaam.

Mama Obama alisema kuwa wake Wa Marais wanakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanawasaidia  wanawake na watoto hasa katika upatikanaji Wa elimu na mahitaji mengine muhimu.

"Jana nilitembelea  makumbusho ya taifa, nilikutana na watoto  ambao  baadhi yao walikuwa ni wale wanaosomeshwa na Mama Kikwete , niliongea nao watoto hawa wanapatiwa bure elimu, chakula na maladhi hakika nampongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya", alisema Mama Obama.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mama Kikwete alisema kuwa wake wa Marais waliohudhuria mkutano huo wanawawakilisha wanawake wa Afrika ambao wanahitaji kusaidiwa katika mambo ya afya,  elimu na ujasiriamali.

Mama  Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)  alisema kuwa katika mkutano huo washiriki watapata nafasi ya kubadilishana ujuzi wa kazi  na kutembelea hospitali ya Kansa ya Ocen Road,kituo cha Mabinti na hospitali ya CCBRT ambako watajionea jitihada kubwa zinazofanywa na watanzania za kuisaidia jamii inayowazunguka.

Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo anaamini kuwa washiriki watarudi katika nchi zao na kuweza kukubaliana na Serikali zao pamoja na wadau Wa wengine kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuimarisha bara  la Afrika.

Mkutano huo wa siku mbili   umeandaliwa na Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya wake Wa Marais wa Afrika na Mke wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie Blair.

Mada kuu ni wekeza kwa wanawake imarisha Afrika lengo l ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa Afya  kwa wanawake, upatikanaji Wa elimu na uchumi katika Afrika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.