MAMA PINDA APONGEZA TAASISI YA TARWOC DROP-IN, CHINI YA MBUNGE MNG'ONG'O IRINGA







Mke  wa waziri mkuu mama Tunu Pinda ( wa tatu kulia) akiwa na meneja  wa kituo kulia Pendo Luoga katibu wa UWT mkoa  wa Iringa Christana Kibiki kushoto ni mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo, Mkurugenzi wa kituo Bi Lediana Mafulu Mng'ong'on mjumbe na Bw .Magoti wa kituo hicho pia
...............................................................................................
Na  Francisgodwin Blog -Mzee  wa matukio daima
KE wa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano  wa Tanzania  mama Tunu Pinda amepongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na kituo  cha TARWOC DROP-IN cha mkimbizi katika Manispaa ya |Iringa   kinachoongozwa mkurugenzi wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu Mng'ong'o kwa kazi nzuri

Mama  Pinda alitoa pongezi hizi juzi baada ya kutembelea  kituo hicho na  kupokea pongezi nyingi kutoka kwa baadhi ya  wanaume ambao  walikuwa wakiongoza kwa unyanyasaji  wa kijinsia kwa wake  wao na wanawake  waliokuwa wakinyanyasika na  waume zao ambao kwa sasa  wameungana na kuishi kwa amani.

Akitoa pongezi hizi kituoni hapo mama  Pinda alisema kuwa  jitihada zinazofanywa na m bunge Mng'ong'o katika  kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia na kudumisha mausiano kwa wanandoa ni hatua  ya kupongezwa na kila mtanzania na angetamani  kuona  vituo kama hivyo vinaanzishwa nchi nzima.

Tunu Pinda alisema kuwa suala la ukatili wa kijinsia  kwa wanawake  limeendelea  kuchukua  kasi kubwa na kuwa  bila jitihada kama hizo za TARWOC katika kutoa elimu upo uwezekano  wa watoto na  wanawake  kuendelea kunyanyasika zaidi.

Hivyo alisema kuwa ili Tanzania kuendelea  kuwa  nchi ya amani  ni vema  suala la  amani likaanzia katika familia kwa wanandoa kujenga utamaduni wa kupendana na kuela familia badala ya kutengana na kusababisha familia kuishi katika mazingira  duni.

Hata hivyo mama Pinda amekubali  kuendelea  kuwa karibu na kituo hicho ili  kuwezesha kujulikana zaidi na kuipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa chini ya mkurugenzi wake Terresa Mahongo kwa kuendelea  kuwa karibu na kituo  hicho bora nchini Tanzania.

Kwa upande wake meneja  wa kituo hicho Pendo Luoga alisema kuwa toka kituo hicho kimeendelea  kupata mafanikio makubwa katika kuwasaidia  watu wanaonyanyasika bila kujali wapi  wanatoka .

Huku afisa mkuu kituo hicho  cha  TARWOC DROP- IN BenidickKibiki akizsema kuwa  kituo chake kimehudumia zaidi ya waathirika 1500 wa unyanyasaji na ukatili wa kijisia, na tatizo kuu likiwa ni uwepo wa mila na destuli potofu, uchumi mdogo pamoja na unywaji wa pombe.

"Tatizo hili linatokana na baadhi ya mila na destuli zetu zilizopitwa na wakati, hasa kwa hili la kujiona sisi wanaume kama ndiyo kila kitu, lakini suala la uchumi nalo linachangia ukatili na unyanyasaji, mtu mwanaume au mwanamke mwenye kipato duni anafanyiwa unyanyasaji kutokana na hali yake duni, la tatu ni kukosekana kwa elimu miongoni mwa jamii, kwani baadhi ya wananchi hawana elimu ya namna ya unyanyasaji," Alisema Kibiki.

Aidha aliongeza kuwa changamoto inayokikabili kituo hicho cha TARWOC DROP- IN cha Mkimbizi ni kukosekana kwa ausafiri wa gari, na hivyo kushindwa kuwafikia wananchi waishio maeneo ya mbali na kituo.

Kibiki alisema Kata 16 zilizopata baiskeri hizo ni kutoka ndani ya Manispaa ya Iringa huku Kata 4 za Iringa vvijijini ambazo ni Kata ya Mseke, Ifunda, Kihologota na Kata ya Kising'a.
Huku viongozi wa  serikali ya mtaaa huo wakudai kuwa hatua ya kituo hicho kukabidhi usafiri kwa mabalozi ni kusaidia kupingana na ukatili Manispaa ya Iringa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bi Mahongo alisema kuwa jitihada zinazofanywa na kituo hicho zimeivutia  halmashauri hiyo hivyo  wamelazimika kutoa ardhi zaidi ili kujengwa  kituo  kikubwa kitakachowezesha  huduma hiyo kuboreshwa zaidi.


Kwa upande  wake mbunge Mng'ong'o mbali ya kump;ongeza mama Pinda  bado alisem akuwa lengo lake ni kuhakmikisha mkoa wa Iringa na Tanzania  kunakuwepo amani na hakuna mwanake  wala mtoto anayenyan yasika.

Siku mbayo  shirika lilionyesha mfano kwa  kutoa Baiskeli kwa watenda kazi wake
Mbarozi wa Kata 20 wakisubiri kukabidhiwa usafiri wa Baiskeri, nje ya kituo cha shirika la TARWOC DROP IN.    
 Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki, akikabidhi Baiskeri kwa mabarozi wa Kata, kutoka Manispaa ya Iringa na Iringa Vijijini.
Baadhi ya mabarozi wakiwa na Baiskeri zao, baada ya kukabidhiwa rasmi na naibu Meya wa Manispaa ya Iringa

 Pendo Luoga (kushoto) Meneja wa kituo cha TARWOC DROP IN- Mkimbizi na Benedict Kibiki (mwenye suti) Ofisa mkuu wa shirika la TARWOC DROP IN- Wakishangilia baada ya makabidhiano hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA