MAN CITY YATENGA PAUNI MILIONI 28 KUMSAJILI JOVETIC

IMEWEKWA JULAI 16, 2013 SAA 3:24 ASUBUHI
KLABU ya Manchester City ipo mbioni kumnunua kwa Pauni Milioni 28, nyota wa Fiorentina, Stevan Jovetic.
Pamoja na hayo, City imepata pigo katika mpango wake wa kumsajili Alvaro Negredo, baada ya rais wa Sevilla, Jose Maria del Nido kuonya kwamba hakuna hata asilimia moja ya uwezekano wa dili hilo kufanikiwa.
Kocha mpya, Manuel Pellegrini anataka kusajili washambuliaji wawili kuziba pengo la wachezaji walioondoka hivi karibuni, Carlos Tevez na Mario Balotelli.
In and out: Alvaro Negredo's move to Man City has hit the skids, but Stevan Jovetic is on the verge of joining
In and out: Alvaro Negredo's move to Man City has hit the skids, but Stevan Jovetic is on the verge of joining
Ndani na nje: Alvaro Negredo anakwenda Man City, lakini Stevan Jovetic yuko njia panda
Shopping: New City manager Manuel Pellegrini is keen to strengthen his attacking options this summer
Dukani: Kocha mpya wa City, Manuel Pellegrini anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji majira haya ya joto

City imekuwa kwenye mazungumzo na Fiorentina juu ya Jovetic kwa muda sasa, lakini inafahamika klabu hizo mbili hatimaye zimekubaliana biashara hiyo kwa Pauni Milioni 23, ambayo itapandisha kiwango cha malipo ya posho hadi Pauni Milioni 5.
Awali, ilivumishwa Fiorentina hawatamuuza mwanasoka huyo wa kimataifa wa Montenegro, mwenye umri wa miaka 23, kwa dau la chini ya Pauni Milioni 28.
City bado ina matumaini ya kumsaini Negredo lakini inaonekana kushindwa kufika dau ambalo wanataka Sevilla, Pauni zisizopungua Milioni 20.
Del Nido alithibitisha jana kwamba klabu hizo mbilo zinapishana katia dau: "Aidha walipe tunachikitaka au mchezaji abaki Sevilla kwa miaka mingine mitatu,". 
Wakati huo huo, City imesema beki Aleksandar Kolarov hatajiunga na Juventus licha ya taarifa kwamba watasikiliza ofa. 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 inaaminika anataka kuondoka, baada ya kupoteza nafasi yake katika beki ya kushoto kwa Gael Clichy, lakini wakati Maicon akijiandaa kujiunga na Roma kwa Pauni Milioni 4, City inataka kumbakiza Kolarov.
Staying put: Manchester City are confident they can keep Aleksandar Kolarov out of Juventus' clutches
Anabaki tu: Manchester City inajiamini itambakiza Aleksandar Kolarov asiende Juventus

Missing man: Carlos Tevez has already completed a switch to the Italian club
Ametoweka: Carlos Tevez tayari amehamia Italia 
Kuondoka kwa Maicon ina maana kutapunguza bajeti ya mishahara ya klabu hiyo kwa Pauni Milioni 40 majira haya ya joto kwani Mbrazil huyo alikuwa anachukua Pauni 100,000 kwa wiki Uwanja wa Etihad, wakati pia Kolo Toure, Wayne Bridge na Roque Santa Cruz, nao wameondoka kama wachezaji huru.
Inakisiwa uhamisho wa Tevez Juventus umeokoa kiasi cha Pauni Milioni 17 City katika bajeti ya mishahara na posho huku klabu sasa ikitaka kufuata sheria ya matumizi mpya ya fedha kiungwana.
Inaonekana hivyo kwa sababu Jovetic na Negredo wataigharimu klabu hiyo Pauni Milioni 50 baada ya kumsajili kwa Pauni Milioni 15, Jesus Navas na Pauni Milioni 30 kwa Fernandinho. Mbrazil huyo aliichezea mechi ya kwanza City katika ziara ya Afrika Kusini na ana matumaini ya kupata mafanikio chini ya Pellegrini licha ya kipigo katika mechi ya kwanza.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*