Mkuu-wa-Jeshi-la-Magereza-nchini-CGP-John-Minja
---
Jeshi la Magereza Tanzania Bara linapenda kuufahamisha Umma kwamba mnamo tarehe 23 Julai, 2013 Maafisa wanne ambao ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro, Sajenti Ketto Ramadhani, Koplo Silyvester Dionice na Wada Richard Barick wa Gereza Kiteto  Mkoa wa Manyara walikamatwa na askari wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Kati wakiwa na gari la Jeshi la Magereza pamoja na silaha likiwa limepakia nyara za serikali. Dereva wa gari hilo  Sajenti Ketto Ramadhan  alitoroka na kutelekeza gari hilo na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta. 

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na maadili ya Jeshi la Magereza pamoja na sheria za  uwindaji wa wanyama pori. Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Magereza limechukua hatua zifuatazo:-
    i.        Askari 3 waliohusika wamefukuzwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza na watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika.

   ii.        Afisa Mrakibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro amefunguliwa mashtaka ya kinidhamu na kusimamishwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza hadi maamuzi ya Mamlaka ya kinidhamu inayomuhusu yeye (Disciplinary authority) itakapotoa maamuzi dhidi yake. Kwa sasa amezuiliwa Kituo cha Polisi Babati kusubiri kufikishwa Mahakamani upelelezi wa Polisi utakapokamilika.

 iii.        Mkuu wa Gereza Kiteto Mrakibu wa Magereza Ally Ramadhani Sauko kwa kutumia madaraka yake vibaya amevuliwa uongozi na kuhamishiwa Ofisi ya Mkuu wa Magereza Manyara, akisubiri maamuzi ya Mamlaka ya kinidhamu inayomuhusu yeye (Disciplinary authority) kufuatia mashtaka ya kinidhamu yaliyofunguliwa dhidi yake. 
Imetolewa na 
Kitengo cha Habari Ofisi ya Makao Makuu ya Magereza 
Tanzania Bara
26 Julai 2013

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*