NMB NA JITIHADA ZA KUSAIDIA SEKTA YA KILIMO TANZANIA

NMB kwa kupitia idara yake ya biashara za Kilimo (Agribusiness Department) leo imetoa ripoti mbili;
1.       Utafiti wa kujua kama mfumo wa stakabadhi mazao ghalani (Warehouse Receipt Financing Sytem) una manufaa kwa wakulima au la? Utafiti umethibitisha kuwa mfumo una manufaa kwa wakulima japokuwa kuna changamoto bado. Mfano wakulima wa kahawa wanaouza mazao yao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani wanapata zaidi ya asilimia 30% ukilinganisha na wale wasiotumia mfumo wa stakabadhi ghalani.
2.       Utafiti wa sekta ya sukari unaonesha kuwa Tanzania inatumia wastani wa tani 520,000 kwa mwaka (ikiwemo sukari kwa matumizi ya viwanda) kati ya hizo uzalishaji ni tani 300,000 na kiasi cha tani 220,000 zinaingizwa kutoka nje kwa mwaka.  Utafiti umeonesha kwamba Tanzania inaweza kuzalisha kiwango cha kutosheleza mahitaji ya nchi iwapo kutakuwa na kilimo cha umwagiliaji, miche bora ya miwa, pembejeo za kilimo zilizo bora ikiwemo mbolea pamoja na mazingira bora ya uwezeshaji (enabling environment) wa sekta ya sukari.
Maofisa wa NMB  Idara ya biashara ya Kilimo, kwanza kulia ni Sierk Plaat ambae ni  Mchambuzi Mwandamizi toka benki ya Rabobank, Robert Paschal Mkuu wa Idara Mikopo ya Kilimo NMB na Carol Nyangaro Mtafiti, Mchambuzi  wa mambo ya kilimo wakionyesha kitabu ambacho kimebeba ripoti ya mfumo wa stakabadhi  ghalani


 Mkuu wa Idara ya biashara za kilimo NMB, Robert Paschal (kati) akiongea na waandishi wa habari na kuwasilisha ripoti ya biashara za kilimo zifanywazo na Benki  ya NMB
 Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria  hafla ya uwasilishaji wa ripoti ya biashara ya kilimo
Sehemu ya maofisa wa NMB wanaoshiriki Maonesho ya Biashara yanayoendelea

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

𝙂𝘼𝙈𝙊𝙉𝘿𝙄 𝙆𝘼𝘾𝙃𝙀𝙕𝘼 𝙆𝙄𝘽𝙄𝙉𝙂𝙒𝘼.