NMB YAWEZESHA MKUTANO WA WASAMBAZAJI MAFUTA NA GESI NCHINI TANZANIA
Mwishoni
mwa wiki NMB ilifadhili mkutano wa makampuni na taasisi ambazo wamepewa
dhamana ya uchimbaji na usambazaji wa mafuta na gesi nchini. Mkutano
huo ulifanyika katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam kwa
siku mbili ukiambatana na maonyesho ya biashara kutoka makampuni tofauti
nchini Tanzania.
Dhumuni
kubwa la mkutano huu lilikuwa ni kutengeneza mahusiano baina ya
wafanya biashara na kujadili jinsi ambavyo huduma zitolewazo na
makampuni na taasisi zilizopewa dhamana ya uchimbaji na usambazaji wa
mafuta na gesi nchini zinavyoweza kuisaidia jamii husika.
Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Miamala kwa Taasisi NMB, Gerald Kamugisha
akielezea jinsi NMB inavyoweza kusaidia makampuni na taasisi mbali mbali
zinazosambaza mafuta na gesi nchini Tanzania.
Kamishina wa Nishati na masuala ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hosea Mbise,akimkabidhi cheti Mkuu wa kitengo cha huduma za miamala kwa taasisi NMB, Gerald kamugisha kwa udhamini ambao NMB umetoa ili kufanikisha mkutano huo.
Meneja
ukuzaji wa biashara NMB, Masato Wasira akiwaelezea baadhi ya washiriki
wa mkutano huo juu ya huduma zitolewazo na benki ya NMB.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wakisikiliza kwa makini.
Comments