OMBAOMBA, WAMACHINGA WAREJEA TENA JIJINI BAADA YA OBAMA KUONDOKA

  Ombaomba akiwa amekiuka amri ya Serikali kwa kurejea jijini na kuendelea na kazi yake kama alivyonaswa na kamera yetu karibu na Mnara wa Askari, katikati ya Jiji la Dar es Salaam  juzi. Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam iliwapiga marufuku ombaomba na wafanyabiashara ndogondogo kufanya shughuli zao katika maeneo mbalimbali ili kuweka mazingira safi hasa wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama. Pia Serikali iliwataka wafanyabiashara hao waliokuwa wametimuliwa katika maeneo yasiyo rasmi kwa biashara wasirudi. (PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA)
Wafanyabiashara ndogondogo wakiendelea na biashara zao baada ya kurejea tena katika eneo la Posta Mpya, jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA MDAU KHAMIS MUSSA
Wauza maji na soda wakiwa kazini jana katika Mtaa wa Azikiwe, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
 Wateja wakipata huduma ya kutoa na kutuma fedha kwa njia ya mitandao ya simu jana katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Vibanda vinavyotoa huduma hizo, viliondolea wakati wa ziara ya Rais Obama nchini.
 Wafanyabiashara ndogondogo wakiendelea na biashara zao baada ya kurejea tena katika eneo la Posta Mpya, jijini Dar es Salaam juzi.

Wauza vocha na wang'arisha viatu wakiwa kazini katika Mtaa wa Samora, Dar es Salaam

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*