Rais Wa Marekani Barack Obama Akutana na Kuhutubia watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali yaliyowekeza Afrika Juu ya Kuimarisha Fursa Za Ushirikiano Kati ya Marekani na Afrika katika Uwekezaji Kwenye Sekta Mbalimbali za Maendeleo.

 Rais wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wafanyabiashara jana jijini Dar es salaam juu ya mpango wa Nchi yake wa kufungua milango ya ushirikiano na uwekezaji kwa Nchi za Afrika Mashariki katika sekta mbalimbali na hivyo kuongeza kiwango cha bidhaa ya Afrika Mashariki zinazoingia nchini Marekani.
Rais wa Marekani Barack Obama akiwa katika mkutano jana  jijini Dar es salaam wa kujadiliana na watendaji wakuu(CEO) wa Makampuni mbalimbali yaliyowekeza Afrika juu ya kuimarisha fursa za ushirikiano kati ya Marekani na Afrika katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam
---
Na Eleuteri Mangi—MAELEZO.Dar es salaam
 
Serikali ya Marekani imeahidi kufungua ukurasa mpya kwa Nchi za Afrika Mashariki kwa kuongeza uwekezaji katika sekta mbalimbali ili kuinua uchumi wan chi hizo.
 
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dar es salaam na Rais Barack Obama kwenye hotuba yake kwa wafanyabiashara wakati wa ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.
 
Alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza kiwango cha bidhaa kutoka Nchi za afrika Mashariki kuingia nchini Marekani na hivyo kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kwa manufaa ya pande zote.
 
 “Sasa ni wakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwekeza nchini Marekani  ili kuongeza mauzo yake nchini Marekani hadi ifike asilimia 40,” alisema Rais Obama.
 
Aliongeza kuwa pia ushirikiano huo unapaswa kuboresha utoaji wa mizigo katika bandari ya Dar  es salaam na Mombasa  kwenda nchi zisizo na bandari ili kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini.
 
Akizungumzia hotuba ya Rais Obama Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye viwanda nchini (CTI) Felix Mosha alipongeza hotuba hiyo kwa kufungua ukurasa mpya kwa nchi za Afrika na Marekani kwa kuonyesha kuwa wakati wa kutegemea misaada umepitwa na wakati badala yake ni kushirikiana katika uwekezaji.Katika mkutano huo kiasi cha wafanyabiashara 170 walihudhuria mkutano huo .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.