RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AONGOZA MAZISHI YA WANAJESHI LEO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (wa tatu kulia) akijumuika na Vingozi na Waislamu wengine katika kuwaswalia  Merehemu Sgt. Shaibu Shehe Othman, na Cpl Mohammed Juma Ally katika Msikiti wa Nuru Muhammad, Mombasa mjini Unguja leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
 Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakibeba Jeneza la mwili wa Marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, baada ya kuwasili mjini Zanzibar akiwa ni miongoni mwa wanajeshi 7 waliouwawa kwa kupigwa risasi Jimbo la Darfur nchini Sudan hivi karibuni.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akitia udongo katika kaburi la Marehemu Sgt. Shaibu Shehe Othman, aliyezikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe mjini Unguja. 
 Baadhi ya Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na Ndugu na Jamaa wa marehemu Sgt Shaibu Shehe Othman, na  Cpl Mohammed Juma Ally wakishiriki mazishi hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati) na Viongozi na Waislamu, wakiangalia  Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania, walipokuwa wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Sgt. Shaibu Shehe Othman, wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Mwanakwerekwe leo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI