Muasisi wa Taasisi ya Strakey Hearing Foundation, Bill Starkey akimhudumia mtoto Lissa Frank (9) ambaye alikuwa kiziwi tangu kuzaliwa na kuweza kusikia baada ya kupata tiba na huduma ya kuwekewa kifaa maalumu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika Hospitali ya Seliani, mkoani Arusha
Nyota wa mchezo wa mpira wa miguu wa Marekani (American Football) Rays Lewis akimpa Rais Jakaya Kikwete zawadi ya kofia yenye nembo ya timu yake wakati nyota huyo alipomtembelea Rais Kikwete mjini Arusha jana. Nyota huyo yuko nchini ambapo ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa huduma kwa wagonjwa wenye ulemavu wa kusikia inayotolewa na Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani.Wagonjwa zaidi ya 3500 wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo inayotolewa bure na taasisi hiyo. (PICHA NA FREDDY MARO)
Nyota wa mchezo wa mpira wa miguu wa Marekani (American Football) Rays Lewis akimpa Rais Jakaya Kikwete zawadi ya kofia yenye nembo ya timu yake wakati nyota huyo alipomtembelea Rais Kikwete mjini Arusha jana. Nyota huyo yuko nchini ambapo ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa huduma kwa wagonjwa wenye ulemavu wa kusikia inayotolewa na Taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani.Wagonjwa zaidi ya 3500 wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo inayotolewa bure na taasisi hiyo. (PICHA NA FREDDY MARO)
WALEMAVU WA KUSIKIA
WANUFAIKA NA HUDUMA ILIYOTOLEWA NA TAASISI YA STARKEY HEARING FOUNDATION.
Na.Freddy Maro,Seliani Arusha.
Julai, 7 ,2013
Zaidi ya Watanzania 3500 wenye maradhi ya kusikia
wanatarajiwa kunufaika kwa huduma ya tiba inayotolewa na Taasisi ya Starkey
Hearing Foundation yenye makao yake jijini Washington nchini Marekani.
Muasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing foundation
Bwana Bill Austin Starkey ameyasema hayo wakati wa
kliniki maalumu ya kuwatibu watu wenye maradhi mbalimbali ya kusikia iliyokuwa
ikifanyika Katika hospitali ya Seliani mjini Arusha baada ya kutoa huduma hiyo
katika miji ya Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Nimefurahishwa sana na kutiwa moyo kwa kazi tuliyoifanya
ya kuwahudumia watu na kuwawezesha kusikia ambapo wengine ndiyo wameweza kusikia
kwa mara ya kwanza tangu walipozaliwa.Furaha yao ni kitu cha kutia moyo sana
katika juhudi zetu.Madaktari wa kitanzania tulioshirikiana nao wamefanya kazi
kubwa na nzuri” alisema Bwana Starkey ambaye ameambatana na timu ya wataalamu na
watu mashuhuri kutoka nchini Marekani ambao wametoa misaada mbalimbali
kugharamia kampeni hiyo.
Bwana Starkey amesema kuwa watu wengi walijitokeza wakati
wa kliniki hiyo maalumu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuongeza kuwa
katika siku tatu walizokuwa mjini Arusha wagonjwa zaidi ya 600 walipatiwa huduma
hiyo ya matibabu kwa kuwekewa vifaa maalumu katika masikio yako na
kuwawezesha kusikia vyema na kusema kila mwaka shirika lake litafanya mipango ya
kuhakikisha kwamba huduma hiyo inakuwa endelevu.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wazazi wenye furaha
baada ya kuona watoto wao wenye umri kati ya miaka mitano na kumi wakiweza
kusikia vyema kwa mara ya kwanza katika maisha yao baada ya
kupatiwa matibabu kwa kuwekewa vifaa maalumu katika masikio yao huduma ambayo
imetolewa bure na shirika hilo na isingekuwa rahisi kuipata kwa watu wengi walio
na kipato cha chini.
Bwana Bill Austin Starkey aliwashukuru wafadhili
mbalimbali waliowezesha mpango huo wa matibabu kufanikiwa na
kuongeza kuwa falsafa ya taasisi yake ni “Ili Dunia ipate kusikia” imeweza
kutekelezwa kwa vitendo kwa sababu anaamini kuwa kukiwa na nia ya
dhat na moyo wa kushirikiana kutekeleza jambo fulani mafanikio ni bayana na
mabadiliko mengi chanya yatawezekana katika ulimwengu.
Bill Austin Starkey na mkewe Tani Austin
ambaye ni muasisi mwenza wa taasisi hiyo pamoja na washirika wao wanatarajia
kwenda nchini Malawi kutoa huduma kama hiyo na baadaye kurejea tena nchini kutoa
huduma kabla ya kuondoka kurejea nchini marekani.
Mmoja wa wataalamu wanaotoa huduma katika kliniki hiyoDkt.
Ron Brouillete alisema mbali na kuzaliwa na ulemavu wa kutosikia wangojwa
wengine waliotibiwa katika kliniki hiyo walipata madhara ya kutosikia kutokana
na matumizi holela ya dawa ya kutibu Malaria aina ya Quinine.
“Napenda kutoa ushauri kwa madaktari na wahudumu katika
sekta ya afya kuepuka kuwapa dawa ya Quinine wagonjwa wa Malaria.Dawa hii
itumike kwa uangalifu mkubwa na pale ambapo dawa nyingine zimeshindwa kumtibu
Mgonjwa,” alisisitiza mtaalamu huyo kutoka nchini Marekani .
Mmoja wa wafadhili wa mradi huo anayefuatana na Bwana Bill
Austin Starkey ni mcheza mpira wa miguu maarufu wa
Marekani(American Professional Football) Bwana Ray Lewis ambaye pia anachezea
ligi ya taifa ya mpira wa miguu ya nchi hiyo(National Football League).
Awali Mchezaji huyo alimtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete aliyekuwa mapumzikoni mjini Arusha na kusema kuwa Rais Kikwete ni mmoja
kati ya viongozi mashuhuri barani Afrika wenye maono ya mbali na nia ya dhati ya
kuwahudumia wananchi wake.
“Nimesoma habari
nyingi mambo mangi yenye mafanikio makubwa anayoyafanya Rais Kikwete na
nilipopata fursa ya kuja nchini Tanzania nikatumia nafasi hiyo kuja
kumsalimia,kumsikiliza na kumpongeza.Ni mtu mnyenyekevu sana na nimefurahi sana
kumtembelea na kuongea naye,” alisema nyota huyo wa mpira wa miguu Marekani muda
mfupi baada ya kukutana na Rais Kikwete ambapo alimzawadia kofia yenye nembo ya
timu yake.
Bill Austin Starkey na mkewe Tani Austin waliunda Taasisi
ya Starkey Hearing foundation mwaka 1984 kwa lengo la kusaidia watu wenye
maradhi ya kusikia na mpaka sasa maelfu ya watu katika sehemu mbalimbali duniani
wamenufaika na huduma inayotolewa na taasisi hiyo.
Mwisho
Comments