TBL YASAIDIA MIRADI YA MAJI YA SH. MIL 50 CHUO KIKUU ST. AUGUSTINE NA SH. MIL. 49 MISUNGWI, MWANZA

 Meneja Mauzo wa Na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki wa kwanza (kulia), kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino, Dkt,Charles Kitima, kwa pamoja wakitaka utepe kuzindua moja ya matanki ya kuhifadhi maji,katika chuohicho.Mradi huo umetekelezwa na TBL kwa gharama y ash. Milioni 50.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Dkt Charles Kitima kushoto akimshukuru  Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki, muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa matanki ya kihifadhi maji chuoni hapo jana.Mradi huo wa ujenzi wa mantaki hayo mawili yenye ujazo wa lita 100,000 kila kila mmoja umegharimu sh. Milioni 50.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Dkt Charles Kitima wa nne kutoka kushoto, Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki, wa nne  kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi matanki mawili ya maji kwa chuo hicho.Wa pili kutoka kulia ni Askafu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Askofu Yuda Thadeus  Ruwa’ich.wa kwanza , kulia ni  Askofu Paul Luzoka .kulia kwa Dkt Kitima ni Padri Mwanjonde.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na  Sheria wa TBL, Stephen Kilindo,akizungumza na baadhi ya  wenyeviti  (hapo pichani) wa Vijiji vya Wilaya ya Misungwi ()muda mfupi kabla ya kukabidhi hundi ya sh.49 milioni kwa ajili ya kukarabati visima vya maji wilayani humo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya hiyo, Nathan Mshana  na Meneja Mauzo na Usambazaji a TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Nathan Mshana akizungumza na baadhi ya  wenyeviti wa vijiji  wilayani humo (hawapo pichani), muda mfupi kabla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 49 kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)

  Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa.Malaki Staki akimkabidhi mfano wa hundi Mkurugenzi wa Ufundi wa kampuni ya Nyagama Investment Ltd  Simon Mazuka, kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ukarabati wa visima 20 vya maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Misungwi.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Stephen Kilindo,wa pili ni kutoka kushoto ni Mhandisi wa Maji Wilayani Misungwi,Jumanne Kitiku.Nyuma ya Malaki ni DED wa Halmashauri ya Misungwi, Nathan Mshana na wa kwanza kushoto ni Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo,Pastory Mkaruka.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa Malaki Staki ,akiwa katika picha ya pamoja na wenyeviti wa baadhi ya vijiji vya wilaya ya Misungwi ambao mradi ya ukarabati wa visima utakaoanza kutekelezwa mapema mwezi huu,  baada ya Kampuni ya TBL kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 49.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*