TIGO KUWANUFAISHA WATEJA WAO KWA KUWAZAWADIA BAJAJI 60 KUPITIA PROMOSHENI MPYA YA 'MILIKI BIASHARA YAKO'

Meneja Mkuu Uendeshaji wa Kampuni inayouza Bajaj ya Fair Deal Auto (PVT) Limited, Anil Dewan (kulia) akimkabidhi Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga moja kati ya Bajaj 60 zitakazotolewa zawadi kwa washindi wa promosheni mpya ya 'Miliki Biashara Yako'inayolenga kuwainua wateja wo kiuchumi. Hafla hiyo imefanyika  Dar es Salaam leo


                                                              Mpinga akikabidhiwa ufunguo
                                                             Mpinga akiwa ndani ya Bajaj
                                                   Wakiwa na furaha baada ya makabidhiano


 
Tigo kuwezesha wateja wake kiuchumi kupitia promosheni ya Miliki Biashara Yako


Dar es Salaam, Julai 18, 2013 – Tigo Tanzania leo imezindua promosheni kabambe iitwayo “Miliki Biashara Yako” inayolenga kuwainua wateja wake kiuchumi kwa kuwapatia fursa ya kushinda usafiri wa Bajaji 60 kwa muda wa miezi miwili ambapo kila siku mteja atajishindia Bajaji moja.

Akitangaza promosheni hiyo katika mkutano na wanahabari, Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga alisema, “Tigo inatambua jukumu lake tulionao katika kuboresha maisha ya Watanzania, na kwa sababu hiyo tumeamua kuzindua promosheni ya aina hii kwa ajili ya kugusa zaidi maisha ya watu. Kwa mara nyingine tena tunawapa wateja wetu sababu ya kutabasamu wakiwa na Tigo kwa kuwapatia nafasi ya kumiliki biashara yao wenyewe kupitia promosheni hii ya “Miliki Biashara Yako”. Hii ni nafasi yakipekee ambapo wateja wetu watapata fursa ya kuwa wajasiriliamali, kujipatia kipato, kutoa ajira, pamoja na kutoa huduma ya usafiri wenye gharama nafuu kwa jamii.”

Wateja wa Tigo wanaweza kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa wateja wengi wanafurahia promosheni hii, mteja hahitaji kuweka vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja ili kushiriki, anaweza kuongeza salio kidogo kidogo hadi kufikisha kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza kuingia kwenye droo. Vile vile mteja anaweza kuongeza salio mara nyingi awezavyo ili kujiongezea nafasi zaidi ya kujishindia Bajaji. Pamoja na hayo, ili kuwapatia urahisi zaidi wateja, bado mteja anaruhusiwa kuongeza salio pitia namna zote zile ikiwemo Tigo Rusha, Tigo Pesa au kwa vocha ya kawaida.

“Tunaamini kwamba promosheni hii itawapatia wateja wetu sababu nyingine yakutabasamu. Wateja 60 watakaopatikana washindi watajinyakulia Bajaji mpya kabisa ambapo wataweza kuzitumia kuanzisha biashara zao wenyewe. Biashara ya Bajaji ni biashara yenye faida sana, kwa siku mmiliki wa Bajaji anaweza kuingiza kipato cha kati ya Tsh 25,000 mpaka Tsh 30,000 kwa siku, sawa na Tsh 900,000 kwa mwezi, ambayo ni Tsh 10,800,000 kwa mwaka,” alielezea Mpinga.

Bw. Mpinga alisema kwamba kila Bajaji ina thamani ya Tsh 6,700,000. “Tayari Tigo imechukua jukumu la kulipia leseni ya barabara (road license) na bima ya Bajaji. Kwahiyo mteja atakuwa amebakiwa na jukumu la kuja kuchukua Bajaji yake na kuanzisha biashara yake mara moja,” alimalizia Mpinga.
 

KUHUSU TIGO:

Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26)

Tanzania bara na visiwani.

Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.

Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya <http://www.millicom.com/> Millicom

International Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi  kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko 13 barani

Afrika na Amerika ya Kusini.

"Tabasamu upo na Tigo"
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

 

Amani Nkurlu – Meneja Mahusiano

 

+255 658 870 107 au +255 712 223 839

 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.