UMOJA WA MATAIFA KUPELEKA JESHI KONGO

Umoja wa Mataifa umesema upo tayari kupeleka jeshi katika uwanja wa mapambano huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kukabiliana na Waasi. Hatua inayotokana na malalamiko ya waandamanaji mjini Goma.
Waandamanaji wanalalamika kwamba walinzi wa amani wamekuwa dhaifu katika kukabiliana na vitendo vya waasi katika maeneo hayo.
Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Kongo limeonekana kujiweka kando kabisa wakati wapiganaji waasi wa kundi la M23 likifanya mashambulizi dhidi ya majeshi ya serikali katika eneo kubwa la mashariki la mji wa Goma.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersirky amenukuliwa na shirika la habari la Ufaransa, AFP akisema jeshi la ulinzi wa amani nchini Kongo, MONUSCO  kwa wakati wote katika operesheni zake nchini humo halijajiingiza katika uhasama.
Jeshi lipo katika hali ya tahadhari
A Congolese army soldier walks through the bush, back from an attack position north-west of Munigi, overlooking the front-line, in the east of the Democratic Republic of the Congo on July 15, 2013. Fighting broke out yesterday between M23 rebels and the national army, and continued today, with heavy artillery fire north-west of Munigi and the army claiming to have taken ground. AFP PHOTO/PHIL MOORE (Photo credit should read PHIL MOORE/AFP/Getty Images) Mwanajeshi wa Kongo kwenye doria katika viunga vya Goma
Msemaji huyo ameongeza kusema majeshi ya bado yapo katika hali ya tahadhari na kujitayarisha kujiingiza katika mapigano hayo, kwa kujumuisha jeshi jipya kwa lililopo nchini humo kwa hivi sasa kwa ajili ya kuleta ustawi. Amesema operesheni hiyo inaweza kuwaweka katika hali ya wasiwasi wakazi wa eneo hilo la mashariki ya Kongo, na hasa Goma.
Kwa mujibu wa AFP, tangu jana kumekuwa kimya katika eneo la Goma. Lakini kulikuwa na maandamano katika mji huo, ambapo baadhi ya wamelituhumu jeshi hilo la Umoja wa Matiafa kwa kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa majeshi ya serikali ya Kongo.
Doria yaendelea Goma
Hadi sasa kuna wanajeshi 2,000 kutoka Afrika Kusini, kati ya 3,000 wanaounda jeshi hilo la Umoja wa Mataifa. Idadi iliyobaki kati ya hao inatoka Tanzania na Malawi. Majeshi hayo yanafanya tu, doria na kwamba mpaka sasa hawajafanya shambulizi lolote pamoja na kuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kama inavyoelekeza mamlaka waliopewa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa Umoja huo Nesirky amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesikitishwa sana uhasama mpya katika maeneo ya mji mkuu wa Kivu ya Kaskazini. Kiongozi huyo wa ametaka pande zote husika katika eneo hilo kufanya jithada katika kudhibiti kuongeka kwa mogogoro huo ambao utazidisha matatizo kwa wakazi.
Waasi wa M23 walifanya mashambulizi Jumapili iliyopita ambapo Jeshi la Kongo lilisema kiasi ya watu 130, waliuwawa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI