UN CONGO YAJIANDAA KUKABILIANA NA WAASI WA KUNDI LA M23 WASISONGE MBELE KATIKA MJI WA GOMA.

https://encrypted-tbn3.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcT8MK0N025V2RYdLm-ag-o1BayCjFB5_vwV_Kx7cnnUXvxZWxCGhgKIKOSO cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa kilichoko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimetangaza kuwa, kimejiandaa kikamilifu kupambana na waasi wa M23 ili kuwazuia wasisonge mbele  kuelekea katika mji wa Goma. 

Askari 3000 kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini kina jukumu la kulinda roho za raia mkabala na mashamb
ulio ya waasi wa M23. 

Kikosi hicho ambacho kimeruhusiwa kuwashambulia waasi hao wa M23 kimesema kuwa, kimejiandaa kikamilifu kukabiliana na hatua yoyote ya waasi hao ya kutaka kusonga mbele kuelekea mjini Goma. 

Wakati huo huo, mapigano makali yaliyojiri kati ya majeshi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waasi wa M23 katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita, yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 130 karibu na mji wa Goma, ulioko katika jimbo la Kivu Kaskazini. 

Hayo yamesemwa na Lambert  Mende Omalanga Waziri wa Habari na msemaji wa serikali ya Congo wakati alipozungumza na waandishi wa habari mjini Kinshasa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.