WANAHABARI KUTOKA NCHI ZA AFRIKA CHINI YA SMARTFISH WASHIRIKI ZOEZI LA KUKAMATA SAMAKI WANAOVULIWA KINYUME CHA SHERIA NA VIFAA VYA UVUVI HARAMU.


Baadhi ya Wanahabari wakikusanya net ambazo walizikuta katika moja ya kijiji kilichopo karibu na ziwa Vctoria Kisumu nchini Kenya, net hizo ni maarufu kama kokoro ambazo kwa kutumia net hiyo wavuvi wamekuwa wakizoa mpaka mayai na hivyo kuyaharibu. Baadhi ya samaki ambao walikamatwa katika zoezi la Wanahabari la kukamata samaki ambao wamekuwa wakivuliwa katika ziwa Victoria kinyume cha sheria, Wataalamu wa masuala ya samaki wamese endapo hatua za kudhibiti uvuvi haramu hazitochukuliwa kunauwezekano mkubwa wa samaki kumalizika katika ziwa hilo.

Mmoja wa Askari Polisi akizungumza na wavuvi waliokutwa na net za kuvulia samaki aina ya kokoro ambazo zimepigwa marufuku kutumika.

Wanahabari wakipakia katika gari samaki ambao wamevuliwa kinyume cha sheria baada ya kufanya msako katika maeneo mbalimbali ya Kisumu zoezi hilo lilifanyika usiku kucha na mchana Ziwani na Barabarani.
Wafanyakazi wa Wizara ya Uvuvi Nchini Kenya wakiwa wamebeba tenga la samaki wadogo ambalo walilikamata katika zoezi maalumu ambalo lilishirikisha Wanahabari kutoka maeneo mbambali ya Nchi za Afrika waliokuwa katika mafunzo ya uvuvi wa samaki chini ya Smartfish kulia ni Mwandishi wa habari kutoka Nchini Tanzania Bw Finegani Wasimbey (PICHA NA IPSHA BLOG)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*