Wanahabari watembelea Mradi wa Uranium uliopo chini ya Kampuni ya Manrta Tanzania,Namtumbo Mkoani Ruvuma
Afisa wa
Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa
Uchimbaji Madini aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo
Mkoani Ruvuma,Fredrick Kriel akitoa mada ya maswala ya Usalama Mgodini wakati wa
Semina fupi kwa Baadhi ya Wanahabari waliofanikiwa kutembelea Mradi huo uliopo
pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seluu na kufahamu mambo mbali mbali juu ya
Madini hayo ya Uraniuam.
Afisa wa Kitengo
cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akionyesha moja ya
mambo muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu yeyote awapo
Mgodini.
Meneja Mkuu wa
Maswala ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Mantra
Tanzania,Cornelis Van Den Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo wa Madini ya
aina ya Uranium wakati wa semina fupi na baadhi ya Wanahabari walioweza
kutembelea Mgodi huo leo,na kuweza kujionea na kufahamu mambo mbali mbali juu ya
Mgodi huo.
Mkuu wa Kitengo
ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo akielezea namna
Kampuni yake inavyoweza kutoa kipaumbele katika kusaidia jamii inayouzunguka
mradi huko.
Baadhi ya
Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini wakifatilia mada
zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi huo.Kulia ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda ambaye ameambatana na wanahabari hao,na wa pili
kulia ni Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija
Palangyo.
Sehemu ya
Mandhali ya Mahema ya maofisi ya Kampuni hiyo wakati huu wa Utafiti wa Madini ya
aina ya Uranium.
Wanahabari hao
wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi
huo.
Afisa wa Kitengo
cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akitoa maelezo ya namna
mambo yanavyokuwa pindi wawapo kazini.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Montage,Teddy Mapunda na kushoto ni Mwanalibeneke Othman Michuzi wakisikiliza
kwa umakini.
You might also like:
Comments