WENGER APEWA RUHUSA KUTOA PAUNI MILIONI 40 KUMSAJILI SUAREZ

KOCHA Arsene Wenger amepewa ruhusa kuamua kuhusu usajili ya Pauni Milioni 40 wa Luis Suarez.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool ni kipaumbe cha kwanza katika usajili wa Arsenal majira haya ya joto na timu hiyo ya London tayari imetoa ofa ya awali ya Pauni Milioni 30 iliyokataliwa.
BIN ZUBEIRY imeripoti mapema wiki hii namna ambavyo Gunners wameanza tena mazungumzo na mabosi wa Merseyside juu ya ofa mpya ya Pauni Milioni 35.
Lakini klabu hiyo ya Anfield imeweka wazi kwamba, mchezaji huyo hawezi kupatikana chini ya bei wanayoitaka.
Big money: Arsene Wenger has been given the green light to spend £40m on Luis Suarez
Mkwanja mrefu: Arsene Wenger amepewa ruhusa kutumia Pauni Milioni 40 kwa ajili ya Luis Suarez
Ofa ya Pauni Milioni 40 litakuwa jaribio tosha la kumng'oa Suarez anayetaka kuondoka Anfield majira haya ya joto.
Wakala wa Suarez, Pere Guardiola, alikuwa na majadiliano na Liverpool ambayo imekubali kusikiliza ofa. 
Ofa hiyo itakuwa uamuzi mzito kwa Gunners ambao wanataka kumnasa mchezaji huyo mmoja kati ya watatu inayowataka sana. 
Sambamba na Suarez, Wenger pia anafikiria kuwasajili Gonzalo Higuain na Wayne Rooney.
Clause: Suarez's agent says that if Arsenal bid, Liverpool will be forced to listen
Sokoni: Wakala wa Suarez amesema ikiwa Arsenal itatoa ofa, Liverpool watatakiwa kuwasikiliza
Back to work: Brendan Rodgers and Liverpool are back in pre-season training
Amerudi kazini: Brendan Rodgers na Liverpool wamerejea kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anaamini Suarez ana deni ka wachezaji wenzake - na mashabiki wa klabu - la kubaki Anfield.
"Si kuhusu mimi au klabu, nafikiri mashabiki na wachezaji wenzake kwa kile wanachompa,"alisema.
"Wamekuwa naye kwa shida na raha, na kwa vipindi vyote alivyopitia kwa misimu zaidi iliyopita. Ikiwa kuna yeyote anayedai, ni wao ni wachezaji wenzake, ambao walipambana upande wake, hakika si mimi,".
Interested: Suarez has said he is flattered by interest from Liverpool's Premier League rivals Arsenal
Anateka hisia: Suarez amesema anapagawa na mpango wa kusajiliwa na wapinzani wa Liverpool katika Ligi Kuu England, Arsenal
Having a whale of a time: Arsene Wenger pictured on the club's pre-season tour
Arsene Wenger akiwa kwenye ziara ya timu kujiandaa na msimu
In doubt: The move for Higuain may have fallen flat as Wenger turns his attentions elsewhere
Shakani: Usajili wa Higuain unaweza kukwama, na Wenger amehamishia mawindo yake sehemu nyingine
Wakati huo huo, beki wa Gunners, Bacary Sagna amesema hataondoka Arsenal - na anataka kuthibitisha anastahili Mkataba mpya.
Sagna, mwenye umri wa miaka 30, yupo katika miezi 12 ya mwisho ya Mkataba wake na ana ofa kutoka Paris Saint Germain, Anzhi na klabu za Mashariki ya Kati.
Mfaransa huyo amegoma kusaini Mkataba wa mwaka mmoja zaidi, akiamini anastahili Mkataba mrefu na anajiandaa kuondoka kama mchezaji huyu mwishoni mwa msimu.
Lakini licha ya utata wa Mkataba wake, Sagna amesema anataka kubaki Uwanja wa Emirates na kuthibitisha anastahili Mkataba wa maana.
"NafuraI kuchezea Arsenal. Naipenda timu yangu, najitolea kwa asilimia 100 kwa ajili ya timu na wakati wote naifanyoa mazuri. Bado nipo hapa. 
Here to stay: Bacary Sagna says he wants to remain at Arsenal
Hapa pa kubaki: Bacary Sagna amesema anataka kubaki Arsenal

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.