Baraza Kuu la Wafanyakazi NSSF Lakutana Dar es Salaam

Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii wakiwa katika  picha ya pamoja baada ya mkutano wao wa siku mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii wakiwa katika
picha ya pamoja baada ya mkutano wao wa siku mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.[/caption] BARAZA Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii limekutana kwa siku mbili jijini Dar es Salaam tangu juzi kufanya vikao vyake vya kazi ikiwa ni pamoja na kuangalia utendaji kazi, kupitia mikakati na malengo mbalimbali iliyojiwekea.

Mkutano huo ambao pia umejadili na kupitisha bajeti ya shirika kwa mwaka 2014/15 umeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa NSSF uliopo Katika Jengo la shirika hilo 'WeterFront House' la jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umejumuisha Watendaji Wakuu toka Makao Makuu, Mameneja wa Mikoa, Watendaji wa kuu wa mikoa na wajumbe wengine wanaounda baraza la wafanyakazi la NSSF. 

Jumla ya wajumbe 142 wameshiriki katika mkutano huo uliofanyika kwa siku mbili. Shirika la NSSF ni miongoni mwa mwashirika makubwa ya hifadhi ya jamii nchini yenye vitega uchumi lukuki na vya thamani kubwa vinaochangia kukua kwa uchumi wa taifa. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao. Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao.Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kushoto) akikaimu uenyekiti wa moja ya vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kushoto) akikaimu uenyekiti wa moja ya vikao vya Baraza Kuu la Wafanyakazi la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. Kulia ni Katibu wake.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (kushoto) akizungumza na mmoja wa wajumbe wa  Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano  wao. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (kushoto) akizungumza na mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika hilo katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na mkutano wao.Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani K. Dau (wa kwanza kushoto) akizungumza na baadhi ya  viongozi waandamizi wa shirika hilo, ambao pia ni wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa kikao cha baraza hilo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA