KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YAZINDUA NA KUKABIDHI MIRADI MIWILI YA MAJI MJINI SONGEA


Hawa Ladha meneja miradi Serengeti breweries, Bw Evans Mlelwa meneja mawasiliano serengeti breweries na Bw Joseph Mkirikiti Mkuu wa Wilaya Songea wakizindua miradi ya maji Songea iliyogharimu zaidi ya millioni 140 hivi karibuni.
Kampuni ya Bia ya  Serengeti Breweries kupitia mpango wake wa kusaidia jamii,imekabidhi rasmi mradi wa maji uliopo katika Kituo cha afya cha  Mletele  na kituo cha afya cha Tanga vilivyopo mjini Songea. Mradi huo umezinduliwa rasmi na Mkuu wa  Wilaya Mh. Joseph Mkirikiti ambaye  alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo 

Mradi huo wa maji ambao umegharimu zaidi ya Shilingi milioni 140 za kitanzania unatarajia kukidhi mahitaji ya watu zaidi ya 100,000  wanaohudumiwa na vituo hiyo na jamii inayovizunguka.. Miradi hii kwa kiasi kikubwa utapunguza mfumuko wa magonjwa na vilevile vifo vya watoto na kina mama wajawazito. 

Mradi wa Hospitali ya Mletele unajumuisha kisima , pampu ya maji ya solar na matanki ya kuhifadhia maji ya lita elfu kumi, na mradi wa Na mradi wa maji wa Hospitali ya Tanga  unajumuisha kisim na pampu ya maji ya solar. Visima hivi viwili vinaweza kutoa  lita 72,000 kwa siku. 

Akiongea katika hafla fupi hospitalini Mletele , Bw. Mkirikiti amesema “ Nafarijika sana kuona hospitali hii sasa imepata suluhisho la tatizo la maji walilokuwa nalo hapo awali. Ningependa kuwashukuru sana Serengeti Breweries kwa juhudi zao katika kusaidia shughuli za kijamii na hasa katika upatikanaji wa maji safi na salama na hasa katika hospitali zetu.” 

Kampuni ya Bia ya Serengeti wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia upatikanaji wa maji safi na salama na tayari wamewezesha miradi mbalimbali ya maji kama vile Iringa – Hospitali ya Frelimo, Moshi – Hospitali ya Mawenzi, Dares salaam – Hospitali ya Temeke na ule wa Mkuranga na Sekou Toure mwanza.

Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti , Bwana Evans Mlelwa , amesema “Suala la kuisaidia jamii kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti limepewa kipaumbele na uzito wa hali ya juu na hasa katika kusaidia upatikanaji wa maji safisalama  na pia endelevu.

Serengetti Breweries inatambua umuhimu wa maji kwa binadamu na pia mchango wa maji katika maendeleo ya nchi, kiuchumi na kijamii. Tutahakikisha tunaendelea kuwekeza katika miradi ya maji kwa ajili ya jamii inayotuzunguka ili kuongeza ari ya uwajibikaji kwa maendeleo ya taifa letu na kwa ustawi wa kila mmoja wetu”,ameongeza Bw. Mlelwa.

“Kampuni ya Bia ya Serengeti na EABL Foundation mpaka sasa tumeshawekeza zaidi ya milioni 500 za kitanzania , katika maeneo mbalimbali ambapo zaidi ya watu 450,000 wanafaidika na miradi hiyo”.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA