KATIBU MKUU WA CCM AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA,ATEMBELEA ENEO LA UJENZI MPYA WA BANDARI

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wake kuhusiana na ujenzi wa hatua za awali za bandari ya Kabwe,wilayani Nkasi mkoani Rukwa.
Mmiliki wa Kampuni ndogo ya Kusindika samaki Bwa.Nassor Shibib,akimpa malezo mafupi  Ndugu Kinana namna ya kuhifadhi samki aina ya Migebuka kabla ya kusafirishwa na kuuzwa katika nchi ya Zambia,Congo,Burundi na Rwanda na wafanyabiashara wa eneo la Kabwe.
 Ndugu Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mmiliki wa Kampuni ndogo ya Kusindika samaki Bwa.Nassor Shibib,katika kijiji cha Kabwe,wilayani Nkasi,namna ya kuhifadhi samaki kabla ya kuuzwa katika nchi ya Zambia,Congo,Burundi na Rwanda na wafanyabiashara wa eneo la Kabwe.
 Ndugu Kinana akipata maelezo mbalimbali kuhusiana na suala la uvuvvi katika eneo hilo ambalo linatarajiwa kujengwa bandari
 Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiangalia samaki katika kiwanda kidogo cha kuhifadhia samaki na kuuza katika kijiji cha Kabwe,Wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa  mapema leo,ambapo pamoja na mengine Ndugu kinana alifanya mkutano wa hadhara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 21 katika mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma,ziara hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha Uhai wa chama,kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata ilani ya CCM.
 Samaki aina ya Migebuka ikiwa imeandaliwa kwa ajili ya kukaushwa kabla ya kuhifadhiwa kwenye majokofu  na kusafirishwa maeneo mbalimbali,ndani na nje ya nchi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na  Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini,Mh.Ally Keisy alipokwenda kukagua ujenzi wa bandari ya Kabwe katika hatua za awali  na kujionea shughuli mbalimbali za uvuvi zinazofanyika katika kijiji hicho kabwe.
 Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM katika kijiji cha Kabwe,wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo jioni.
 Katibu Mkuu wa CCM;ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kirando,wilayani Nkasi mapema leo.Kinana alisema kuwa tahakikisha Barabara ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda kijiji cha kabwe itatengenezwa kwa kiwango cha lami."Nitaenda na mbunge wenu kushinikisha suala la barabara hii ili ijengwe kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia sughuli za  kibiashara"alisema.Alisema kuwa maendeleo hayawezi kuja ikiwa miundombinu ni mibovu hivyo atahakikisha analifikisha kwa waziri mwenye dhamana pamoja na mkuu wa nchi ili kazi hyo ifanyike mapema. 

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM,mapema leo jioni katika kijiji cha Kabwe,Wilayani Nkasi.Kinana alisema kuwa, Serikali inatambua  matatizo ya wananchi wa kjijini hapo ikiwemo suala la pembe jeo, maji pamoja na uvamizi wa wavuvi. "Miradi yote inayotekelezwa nchi nzima kwa sasa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010, hatubagui kwakua wote ni watanzania"alisema.Alisema kuwa Serikali inatambua kuwa shughuli kubwa ya kijini hapo ni uvuvi hivyo itajitahidi kuwe na utaratibu wa kuwasaiidia kupata mikopo ili waweze kununua zana za uvuvi ili waweze kujiendeleza.
 Mdau Kamanda wa Matukio Richard Mwaikenda akitafuta taswira mwanana kabisa kwenye mkutano wa hadhara mapema leo mchana katika kijiji cha Kabwe,wilani Nkasi mkoani Rukwa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU