KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA 60 ZA NHC WILAYANI MLELE LEO

 Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe na kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
  Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akifafanua zaidi kuhusiana na mradi huo kwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi leo.
 Meneja Huduma kwa jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),makao Makuu jijini Dar,Bwa.Muungano Sagaya akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake  kwenye uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
 Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akizungumza mbele ya mgeni rasmi,katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kabla ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
 Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh.Rajab Rutengwe akizungumza jambo kabla ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
 Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mh.Rajab Rutengwe kabla ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.



 Katibu Mkuu wa CC,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),mkoa wa Katavi,Bwa.Nehemia Msigwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba 60 za Shirika hilo,katika kijiji cha Inyonga ndani ya Wilaya Mpya ya Mlele mkoani Katavi mapema leo jioni.
========  ======  =====

KATIBU Mkuu wa CCM amelipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kwa kasi ya ujenzi miradi ya nyumba za makazi na biashara kwenye miji mbalimbali hasa makao makuu ya wilaya mpya.

Kinana aliyasema hayo katika mji wa Inyonga wilayani Mlele mkoa wa Katavi wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 60 za shirika hilo.

Alisema uongozi mpya wa NHC umerudisha heshima na hadhi ya shirika hilo kwa kufanya kazi ambazo inapaswa kuzitekeleza.Kwa mujibu wa Kinana, katika kipindi cha karibuni NHC, imekuwa ikitekeleza kwa kazi miradi ya ujenzi wa nyumba za viwango mbalimbali ambazo ni muhimu na kimbilio la watu wa kipato cha chini.

"Hii ndio kazi inayopaswa kufanywa na shirika la nyumba ambalo ni tegemeo la wananchi. CCM inatambua kazi mnayoifanya inakupongezeni na kuungeni mkono katika kutekeleza majukumu yenu," alisema.

Akizungumza kuhusu kilio cha kutaka kupunguziwa kodi kwenye vifaa vya ujenzi vya shirika hilo, Kinana alisema hoja hiyo ni muhimu na inayopaswa kusikilizwa na kupewa kipaumbele kwa lengo la kuwasaidia watu wa kipato cha chini.

"Naona hapa kuna hoja ya msingi kwa kuwa hakuna sababu ya kutoza kiwango kibwa cha kodi kama nyumba zinazojengwa zinawasaidia watu wa kipato cha chini wakiwemo watumishi wa umma wenye mishahara midogo," alisema.

Kwa upande wake, Meneja wa NHC mkoa wa Katavi, Nehemia Msigwa, alisema nyumba hizo 60 zitajengwa kwa kipindi cha miezi minane.

Alisema zitakapokamilika, nyumba hizo zitauzwa kwa bei tofauti huku ya juu ikiwa ni sh milioni 54 na ya chini sh milioni 38.

Msigwa alisema nyumba hizo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa NHC kujenga nyumba 15,000 kwa kipindi hadi mwaka 2015.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.