KIKUNDI CHA KINAMAMA OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA WATOA MSAADA KWA WANAFUNZI WA SHULE YA WASIOONA YA MALANGALI MJINI SUMBAWANGA


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wasioona Malangali Mwl. Orthor M. Mkangara akitoa maelezo mafupi ya shule hiyo iliyoanzishwa rasmi mwaka 1998 ambapo mpaka hivi sasa ina jumla ya wanafunzi 71 wengi wao wakiwa wasioona na baadhi wakiwa ni walemavu wa ngozi "Albinism". Alisema kwa sasa shule hiyo inahitajio kubwa na vifaa vya kufundishia pamoja na usafiri kwa ajili ya kurahisisha shughuli mbalimbali shuleni hapo. 

Alisema kuwa zipo changamoto nyingi shuleni hapo ambapo wadau mbalimbali wanakaribishwa katika kusaidia kuzitatua. Aliwashukuru kikundi cha kinamama kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa (pichani kushoto) kwa msaada waliotoa na kuomba wadau wengine kuwa na moyo kama huo katika kusaidia watoto wenye ulemavu hapa nchini. 
Katibu wa Kikundi cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Bi. Joyce Mwanandenje akizungumza kwa niaba ya umoja huo ambapo alisema lengo la ujio wao Shuleni hapo ni kutimiza desturi yao ya kila mwaka ambapo hutembelea makundi ya wahitaji mbalimbali katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Katika salam zao shuleni hapo walitoa msaada wa magodoro 20, Sukari, sabubi na zawadi mbalimbali kwa aijili ya wanafunzi. Kikundi hicho cha Kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa kinaundwa na watumishi wanawake kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Hazina Ndogo, Ukaguzi wa Ndani, Chuo Kikuu Huria na Baraza la Nyumba na Ardhi Mkoa.
Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo wakiimba wimbo mwanana wa kuwakaribisha kikundi cha kinamama Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa walipofika shuleni hapo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA