KINANA AKAGUA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka wa Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma leo.Kinana yupo katika ziara ya siku 5 mkoani humo ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM,Kinana akiwa na viongozi wengeni wakiangalia jinsi watanzania wanavyopata taabu na kunusurika kifo kwa kuvuka kwenye Mtro Malagalasi wakitokea kuuza bidhaa zao na kununua mahitaji mengine katika Soko Buhinja, Kijiji cha Mrambi, Mkoa wa Makamba nchini Burundi. Wananchi hao kutoka Kijiji cha Kibande na vijiji viongine wilayani Buhigwe, Kigoma Tanzania, huenda Burundi kufanya biashara kutokana na upande wa Tanzania kutokuwepo soko kunakosababishwa na kodi nyingi.
 Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha jinsi wananchi wa Tanzania wakivuka mto huo na wengine kuvushwa kwa malipo, wakirudi Tanzania baada ya kufanya biashara upande wa Burundi.




Mmiliki wa Blogu hii ya Kamanda wa Matukio, Kamanda Richard Mwaikenda (wa pili kulia) akiwa na jopo la wanahabari walio kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, wakiwa  katika picha ya pamoja wakati Kinana alaipotembelea Mto Malagalasi ambao ni mpaka  wa Tanzania na Burundi.Kutoka kushoto ni Grace Gulisha, wa Jambo Leo, Seleman Jongo wa gazeti la Uhuru na Bakari Kimwanga wa gazeti la Mtanzania.

Kinana (kulia), Nape (wa pili kulia) wakiwa na viongozi wengine wa CCM wakiondoka katika mpaka huo
Watanzania wakirejea Tanzania kutoka Burundi
 Askari wa JWTZ akilinda mpaka wa Tanzania na Burundi pamoja na wananchi katika Kijiji cha Kibande Tanzania
Soko la Mchana la Buhinja, lililopo katika Kijiji cha Mrambi, Burundi ambapo watanzania wanaenda kuuza bidhaa zao ikiwemo hata mifugo. Kinana ameitaka Serikali ya Tanzania na viongozi walio katika mikoa iliyo mipakani kuanzisha haraka masoko na kuwapa uhuru wananchi wa kufanya biashara bila bugudha na kuzindoa kodi zisizokuwa na maana.
 Msanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni kutoka Burundi wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kibande, Wilaya ya Buhigwe
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akipiga ngoma huku msanii wa ngoma ya Burundi akiruka juu ikiwa ni minjojo yake wakati ngoma hiyo ikitumbuiza
 Mmiliki wa Blog hii ya Kamanda wa Matukio, Kamanda Richard Mwaikenda akipiga ngoma ya asili ya kikundi kutoka Burundi kilichokuwa kinatumbuiza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibande, Wilaya ya Buhigwe, Kigoma.
Kinana akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa kikundi cha akina mama wa Kijiji cha Kibanda, Buhigwe, mkoani Kigoma
 Kinana akihutubia umati wa watu katika Kijiji cha Kibande, Kigoma.

 Askari Polisi wa kike akilinda doria wakati wa ziara katika Kijiji cha Kibande, Buhigwe Mkoa wa Kigoma
Kinana akihutubia katika Kijiji cha
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CNDD/FDD  Mkoa wa Makamba,Burundi, Nishimwe Zenon (kulia)akielezea kwenye mkutano huo jinsi ya kudumisha ushirikiano na CCM ALIPOKARIBISHWA KWENYE MKUTANO WA HADHARA, wilayani Buhigwe.
Kinana akisalimiana na Zenon
Kinana akiwa na viongozi wengine wa CCM,wakitoka kuona kianzo cha Mto Malagalasi ambao ni mpaka wa Tanzania na Burundi eneo la Manyovu, wilayani Buhigwe.
Kinana akisapungia mikono wananchi alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mnanila, Kata ya Manyovu
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mnanila, Manyovu, wilayani Buhigwe.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Walid Kaborou akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mnanila,Kata ya Manyovu.
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mnanila, Manyovu,wilayni Buhigwe.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI