KINANA AZINDUA MRADI MKUBWA W MAJI KASULU

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wawatu mjini Kasulu, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayote kelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM. Kinana ambaye tayari ameshafanya ziara mkoani Rukwa, hivi sasa ameanza ziara mkoani Kigoma.Akiwa Kasulu alizindua mradi mkubwa wa maji  katika Kijiji cha Nyumbigwa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa watu katika Kijiji cha Nyenge, Kata ya Kurugongo wakati wa ziara yake wilayani Kasulu leo ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM. Kinana ambaye tayari ameshafanya ziara
mkoani Rukwa, hivi sasa ameanza ziara mkoani Kigoma. Kinana amesema kuwa atautafutia ufumbuzi  mgogoro wa wananchi na hifadhi ya Kagerankanda kwa kuwashirikisha mawaziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wa Maliasili nia Utalii.Pia akatika Kata ya Titwe alikabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya 500.
Kinana akiwaongoza wanachama wa chama hicho kula kiapo cha utii katika mkutano wa hadhara mjini Kasulu.
Waendesha bodaboda, wamachinga na wafanyabiashara wakisikiliza kwa makini wakati Kinana akizungumza nao kuhusu jinsi ya kuyatatua matatizo mbalimbali yanyowakabili.
Kinana akizungumza na wamachinga , wafanyabiashara na wamachinga katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu TTC, mjini Kasulu.
Kinana akipata maelezo kuhusu ukamishaji wa ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Nyumbigwa, wilayani Kasulu. Mradi huo mkubwa wa maji utakuwa unatoa lita mil. 2 za maji kwa saiku.
Wananchi wakishangilia kupata mradi huo wa maji.
Nifuraha tele kwa wanachi kupata mradi huo wa maji .
Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Migumga katika Kata ya Kurugongo.
Kinana akisalimiana na wananchi alipokuwa akiingia kwenye mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Nyenge, Kata ya Kurugongo, wilayani Kasulu.

Wananchi wakishangilia katika mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Kinana mjini Kasulu
Mbunge wa Viti Maalumu wa CCM Mkoa wa Kigoma, Josephine akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Kasulu.
Mjumbe wa NEC CCM, kutoka Zanzibar, Ali Abeid Karume katika mkutano wa hadhara mjini Kasulu, ambapo alisisitiza kuwepo muungano wa Serikali mbili.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Mnauye akihutubia umati wa watu mjini Kasulu na kuwaponda wapinzani na hasa Chadema ambapo alisema hivi sasa chama hicho kiko mahututi hasa baada ya kukibwaga katika uchaguzi wa udiwani, uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Chalinze na ule wa Chalinze.
Kinana akivishwa vazi la kabila la Waha wakati wa mkutano wa hadhara mjini Kasulu
Kinana akikabidhiwa Hot Pot ya asili kwa ajili ya kuhifadhia chakula
Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Kasulu

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Danny Makanga akielezea utekelezaji wa miradi mbalimbali wilayani humo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*