Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imetoa wito kwa wananchi kujenga utaratibu wa kusoma maelezo ya bidhaa za vyakula zinazouzwa katika maduka mbalimbali nchini ili kubaini nchi zilikotengenezwa bidhaa husika, muda wa matumizi na taarifa za uthibitisho wa bidhaa hizo kutoka mamlaka hiyo ili kuepuka madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa zisizokidhi viwango.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo (kulia) akitoa ufafanuzi wa baadhi
ya bidhaa zilizokamatwa katika ukaguzi maalum kwenye maduka ya kuuzia
vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika jiji la Dar es
salaam zikiuzwa kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi sura ya
219. Wengine ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw.
Raymond Wigenge, na Meneja wa Ukaguzi wa Chakula wa TFDA kanda ya
Mashariki Bw. Emmanuel Alphonce.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam kuhusu ukaguzi maalum wa maduka ya kuuzia
vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika jiji la Dar es
salaam kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi sura ya 219.
----
Na Aron Msigwa-MAELEZO, Dar es salaam
Mamlaka
ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imetoa wito kwa wananchi kujenga
utaratibu wa kusoma maelezo ya bidhaa za vyakula zinazouzwa katika
maduka mbalimbali nchini ili kubaini nchi zilikotengenezwa bidhaa
husika, muda wa matumizi na taarifa za uthibitisho wa bidhaa hizo
kutoka mamlaka hiyo ili kuepuka madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa
zisizokidhi viwango.
Comments