MASHINDANO YA TANZANIA MOVIE TALENTS KUHAMIA KANDA YA KATI MKOANI DODOMA, ZOEZI LA KUTAFUTA WASHINDI KUANZA JUMAMOSI YA WIKI HII

Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza
Hatimaye Kikosi Kazi cha Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ndio waratibu na waandaaji wa Mashindano ya Kusaka vipaji vya uigizaji Tanzania yajulikanayo kama Tanzania Movie Talents (TMT) kinaondoka leo asubuhi Mkoani Mwanza Kuelekea Mkoani Dodoma kwaajili ya kuendelea na shindano la kusaka vipaji vya kuigiza katika Kanda ya Kati.
Ambapo mashindano yatafanyika Mkoani Dodoma katika Ukumbi wa African Dream kuanzia Jumamosi ya tarehe 12 April 2014 kuanzia Saa moja asubuhi hadi tarehe 15 April 2014, kabla ya mashindano hayo kufanyika Mkoani Dodoma mnamo Siku ya Ijumaa tarehe 11 April 2014 kutakuwa na Promo pati itakayofanyika katika Ukumbi wa Disco wa 84 Mjini Dodoma na Wasanii Lulu, Joti, Rich Rich, Monalisa na MC Pilipili watakuwepo ndani ya nyumba.
Mashindano haya yatakuwa ni muendelezo wa mshindano yaliyoanza kufanyika katika Kanda ya ziwa Mkoani Mwanza ambapo Washindi watatu kutoka Mkoani Mwanza wakiwakilisha Kanda ya Ziwa wakiwa wameshapatikana na kila mshindi aliweza kupewa zawadi ya shilingi laki tano kila mmoja na kusubiria kwenda Mkoani Dar Es Salaam kwaajili ya kuungana na washindi wengine Wa kanda zilizobaki kwaajili ya Fainali kubwa itakayofanyika mkoani Dar Es Salaam

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.