Mke wa Rais Jakaya Kikwete Azindua Kampuni ya Vipimo na Matibabu ya Saratani ya Shingo ya Kizazi Kwa Wanawake Wilayani Bahi Dodoma


Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete akiwa na viongozi
mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma walipokuwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya
vipimo na tiba kwa ajili ya ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Uzazi kwa
wanawake iliyofanyika Wilayani Bahi.

Mama Salma Kikwete akisalimiana kwa kugongeana mikono na Wananchi wa
Wilaya ya Bahi alipohudhuria uzinduzi wa kampeni ya vipimo na tiba kwa
ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi.

Mke wa Rais Jakaya Kikwete Mama Salma Kikwete akisalimaiana na Afsa wa
idara ya Afya ya Jamii wa Shirika la DCMC Katrin Boehl ambao
wanashirikiana moja kwa moja kwenye uendeshaji wa mradi wa Saratani ya
Shingo ya Kizazi kwa wanawake, alipofika kuzindua Mradi huo.

Dakitari Bingwa wa Macho wa Ona Network INC inayotoa huduma za Afya ya
Macho Vijijini akimuelezajambo Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma
Kikwete aliyefika Wilayani Bahi Kuzindua Kampeni ya Vipimo na Matibabu
kwa ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Kizazi.

Wanawake wanaosumbuliwa na macho wakiwa katika viwanja vya shule ya
msingi Bahi walipofika kupata vipimo vya macho na magonjwa mengine
vilivyokuwa vikitolewa bure wakati wa uzinduzi wa kampeni ya tiba ya
ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya kizazi inayotolewa bure.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bahi wakiwa na Mabango yenye ujumbe
Tofauti wakati wa uzinduzi wa Vipimo Vya Saratani ya Shingo ya Kizazi
iliyofanyika juzi katika Viwanja vya Shule ya msingi Wilayani humo.

PICHA NA JOHN BANDA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.