Mkufunzi mkuu na meneja wa klabu ya Manchester United David Moyes ametimuliwa.
David Moyes amefutwa kazi baada ya kushikilia usukuni wa klabu hiyo kwa miezi kumi tu.
Moyes,
mwenye umri wa miaka 50, aliteuliwa na Ferguson kumrithi alipostaafu
mwaka jana baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka 26.Klabu hiyo hapo
awali ilikuwa imekataa kuzungumzia udaku wa magezti kuwa Moyes atafutwa
kazi kabla ya msimu kumalizika.
Taarifa
kutoka kwa klabu hiyo imemshukuru Moyes kwa bidii, uaminifu na hekima
aliyoonyesha kocha huyo akiwa mkufunzi wa Manchester United.
Moyes
alichukuwa usukani wa kuifunza Manchester United mwaka uliopita baada ya
aliyekuwa kocha wa siku nyingi Sir. Alex Ferguson kustaafu.
Huku
zikiwa zimesalia mechi nne pekee msimu wa ligi kukamilika Mancheseter
united inashikilia nafasi ya saba kwenye jedwali la msimamo wa ligi hiyo
alama ishirini na tatu nyuma ya viongozi Liverpool.
Klabu
hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa
mara ya kwanza katika kipindi cha takriban miaka ishirini
Comments