Sehemu ya Umati wa watu uliohudhuria tamasha la pasaka mwaka jana katika uwanja wa Taifa.
KAMATI ya
Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, mwishoni mwa wiki iliyopita ilitangaza
viingilio vya tamasha hilo litakalofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam, viti vya kawaida ni shilingi 5000 na watoto 2000.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Alex Msama viti maalum ni
shilingi 20,000 wakati VIP ni shilingi 10,000.Msama alisema hivi sasa
wanaendelea na mchakato wa kufanikisha zoezi la mgeni rasmi katika
tamasha hilo kwani hivi karibuni watakamilisha zoezi la upigaji kura
kumchagua. Msama
alisema mchakato wa kuelekea katika tamasha hilo litakalofanyika jijini
Dar es Salaam Aprili 20 na baadaye mikoa mingine saba hapa nchini.
Aidha
Msama alitoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam kujiandaa na tamasha hilo
ipasavyo kwani lina mlengo wa kurudisha mapato yanayopatikana na
kuyapeleka katika maeneo matatu ambayo yanawahusu, yatima, walemavu na
wajane.
Msama
alisema mipangilio yake ya kuwawezesha wenye uhitaji maalum ni
kuwajengea kituo kitakachokuwa katika eneo la Pugu nje kidogo ya jiji la
Dar es Salaam ambacho kitajulikana kama Jakaya Mrisho Kikwete, rafiki
wa wasiojiweza.
Comments