PICHA:BENKI YA CRDB YAIPIGA JEKI UBALOZI WA TANZANIA MAREKANI KWA AJILI YA MAANDALIZI YA SHEREHE YA MUUNGANO
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na
Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dr. Charles Kimei (kushoto) na Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bwn. Martin Mmari kwenye kikao cha
makabidhiano ya mchango wa CRDB kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani
kwa ajili ya sherehe ya miaka 50 ya Muungano zitakazoadhimishwa kitaifa
Washington, DC April 26, 2014 CRDB kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ilimkabidhi Mhe. Liberata Mulamula fedha taslimu za
Kimarekani dola 5,000 siku ya Ijumaa April 11, 2014. Makabidhiano hayo
yalifanyikia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe.
Liberata Mulamula akisalimiana na Bwn. Saugata Bandyopadhyay CRDB
Deputy Managing Director (operations and customer services)
Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Bwn. Alex Ngusaru Director of Treasery wa CRDB
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bwn. Martin Mmari akimkabidhi Balozi wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kitita cha dola 5,000
katika kikao cha makabidhiano kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania siku ya
ijumaa April 11, 2014.
Comments