RAIS KIKWETE AWATAKA TRA KUKAA NA WADAU KUTAFUTA MAJAWABU YANAYOLALAMIKIWA KUHUSU MASHINE ZA EFD

RAIS KIKWETE
KARATU, Tanzania
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa mashine za electroniki za ukusanyaji kodi za EFD ni lazima ziendelee kutumika nchini na ameagiza viongozi wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA) kukaa chini na wadau na watumiaji wa mashine hizo kuzungumza na kutafuta majawabu yanayolalamikiwa na wadau.

Rais Kikwete amesema kuwa anajua kuwa yapo maneno mengi kuhusiana na mashine hizo lakini Serikali haitarudi nyuma katika matumizi ya mashine kwa sababu dunia nzima inakwenda huko.

Rais, metoa msimamo huo wa Serikali kuhusu EFD asubuhi ya leo, Jumanne, Aprili 22, 2014 wakati alipozunguza kwenye sherehe ya uzinduzi wa Ofisi za TRA mjini Karatu, Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha.

“Najua kuna maneno mengi kuhusu suala hili. Kwa hiyo maelekezo yangu ni kwamba kaeni chini, myajadili matatizo yaliyopo na kupata ufumbuzi. Kama ni suala la bei pia linazungumzika lakini tuhajitaji mfumo huu wa malipo ya kodi,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Kwenye hili tusirudi nyuma kwa sababu tukifanya hivyo, tutakuwa
tunarudi nyuma sana kwa sababu dunia nzima inaelekea huko na hata majirani zetu wote ama wameanzisha mfumo huo ama wanajiandaa kuuanzisha.”

Rais Kikwete amesisitiza: “Hatuwezi kurejea kwenye mfumo ule wa kitumia vijirisiti. Mfumo wa sasa unaifanya kazi ya kukusanya kodi kuwa rahisi kwa Serikali yenyewe na kwa walipa kodi. Najua watu hawapendi kulipa kodi lakini hakuna njia ya jinsi ya kuendelea isipokuwa kwa kulipa kodi”.

Rais Kikwete alikuwa katika ziara ya siku moja kukagua shughuli za maendeleo wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha na kesho atafanya ziara kama hiyo ya siku moja katika Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro.
0 Comments

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*