Rwanda yakumbuka mauaji ya Kimbari

Rwanda inaadhimisha miaka 20 tangu kutokea mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Watu laki nane waliuawa wengi wakiwa wa kabila la Tutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri. Wote waliuawa na watutsi wenye msimamo mkali.
Hii leo Rais Paul Kagame anatarajiwa kuwasha mwenge ambao utasalia hivyo kwa siku 100 , kipindi ambacho mauaji ya kimbare yalifanyika.
Mgogoro wa kidiplomasia umesababisha Waziri wa sheria wa Ufaransa, kujiondoa katika shughuli za kumbukumbu ingawa Ufaransa inasema kuwa balozi wake ataiwakilisa nchi hiyo.

Wengi wa waathiriwa wa mauaji ya Rwanda, walishambuliwa kwa mapanga kwa siku 100. Mauaji hayo yalianza Aprili mwaka 1994, punde baada ya kufariki kwa hayati Rais Juvenal Habyarimana.

Mauaji ya kimbari Rwanda

  • 6 Aprili: 1994: Rais Habyarimana afariki katika ajali ya ndege
  • 7 Aprili: Wanajeshi wa Rwanda pamoja na waasi wawaua wananchi
  • 8 Aprili:Kundi la waasi la (RPF) laanza kupambana
  • 11 Aprili: Maelfu wauawa
  • 17 Mei: Baraza la usalama la umoja wa mataifa lasema mauaji ya kimbari yametokea
  • 22 Mei: RPF yadhibiti uwanja wa ndege wa Rwanda
  • 22 Juni: Mauaji ya watutsi yaendelea licha ya kuwepo wanajeshi wa Ufaransa nchini humo
  • 4 Julai: RPF yadhibiti Kigali
Alifariki wakati ndege yake iliposhambuliwa katika anga ya Kigali na kudunguliwa.
Baadhi ya viongozi wa kidini walihusishwa na ghasia zilizofuata kifo cha Habyarmana.
Mauaji ya kimbari yaliisha mwezi Julai 1994 wakati chama cha RPF, kilichokuwa cha waasi wa Tutsi wakati huo, kilipoingia nchini humo kutoka Uganda na kuchukua uongozi wa nchi hiyo.
Kumbukumbu zinaanza kwa kuwekwa mauwa katika eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo na kufuatiwa na kuwashwa kwa mwenge katika uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali.
Mwenge huo umekuwa ukitembezwa katika nchi hiyo kwa miezi mitatu iliyopita
Viongozi wa kimataifa akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair,aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki na katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Mnamo Jumapili mamia ya watu walihudhuria maombi kuwakumbuka maelfu waliouawa

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*