Serikali yaeleza mipango ya kuendeleza masoko jijini Dar es Salaam

Afisa Uhusiano Manispaa ya Ilala Bi. Tabu Shaibu akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusu mpango wa serikali wa kuendelea kuimarisha Masoko katika Jiji la Dar es Salaam, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa Manispaa hiyo Bw. Athuman Mbelwa.
======  ==== ======
Na Frank  Mvungi- Maelezo
Serikali yaimarisha masoko 18 katika jiji la Dar es salaam katika kukabiliana na Ongezeko la Mahitaji ya Wananchi. Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala Bi Tabu Shaibu wakati wa mkutano nawaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Akifafanua Bi Shaibu amesema masoko makubwa ni 5  ambayo ni Buguruni,Ilala,Ferry,Kisutu na Mchikichini ambapo jumla ya wafanyabiashara  wanaotumia masoko hayo ni 8,432. 
 
Akieleza  zaidi Bi Shaibu alimesema kutokana na Utafiti uliofanywa na Ofisi ya Biashara ya Manispaa ya Ilala mwaka 2009,ilibainika kuwa jumla ya wafanyabishara 21,500 hawana maeneo ya kufanyia biashara na wanatumia hifadhi ya barabara na maeneo yasiyoruhusiwa kufanya biashara.

Kutokana na hali hiyo Bi Shaibu alibainisha kuwa katika bajeti  ya 2013/2014 jumla ya sh.Milioni 240 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ya masoko ya Pugu ,Kigogo fresh,Kiwalani na Kinyerezi ambapo wakandarasi wameshaonyeshwa maeneo ya ujenzi  kwa njia ya zabuni.

Katika hatua nyingine Bi shaibu alisema sh. Milioni 170 zimetumika kuboresha soko la Samaki feri kwa ajili ya ujenzi wa  zoni ya kukaangia samaki baada ya kuungua. Pia sh. Milioni 75 zilitumika. kuboresha mifereji ya maji taka,ukarabati wa meza 23 za kunadia samaki,kuzibua mitaro ya maji taka na maji ya mvua.

Ni jukumu la wafanyabiashara wote kuzingatia usafi kwa kuhakikisha kuwa taka zinazozalishwa katika masoko yote zinahifadhiwa katika maeneo husika na kutunza mazingira ya maeneo ya masoko ili kuwalinda watumiaji wa huduma zinazotolewa katika maeneo hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI