Soma Taarifa Kwa Umma Kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma:Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inawatahadharisha wananchi wote, ndani na nje ya nchi kujihadhari na watu wanaotumia jina la Utumishi kuwaibia fedha na kupoteza muda wao kufuatilia jambo ambalo halipo.


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 
OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
TAHADHARI
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inawatahadharisha wananchi wote, ndani na nje ya nchi kujihadhari na watu wanaotumia jina la Utumishi kuwaibia fedha na kupoteza muda wao kufuatilia jambo ambalo halipo.

Watu hao wanatumia majina yafuatayo katika mitandao:

Saving Foundation Loans na Jakaya Foundation kwa anuani
http://savingfoundation.wapka.mobi/index.xhtml na kuelekeza kuwa Makao Makuu yapo kwenye jengo la UTUMISHI.

Namba za simu zIfuatazo zimekuwa zikItumika kuwatapell wananchI watume fedha; 0715-373307, 0656-037520 na 0762-269376.

Wananchi epukeni kurubuniwa na watu hao kwani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma haijishughulishi na kutoa mikopo ya aina yoyote kwa wananchi.
Tangazo limetolewa na 
Katibu Mkuu, 
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma. 
2 Aprili, 2014 
Mawasiliano: permsec@utumishLgo,
S.L.P 2483 
Dar es Salaam,
Simu, (255) 22 2118531-4 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA