TIMU YA SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA KUIGIZA LIJULIKANALO KAMA TANZANIA MOVIE TALENTS YAWASILI SALAMA MKOANI DODOMA TAYARI KWA ZOEZI LA USAILI LITAKALOANZA NA PROMOTION PARTY NDANI YA CLUB 84 HAPO KESHO
Hatimaye
kikosi kazi cha Proin Promotions Limited kimeshawasili mkoani Dodoma
tayari kwa Kazi ya Kusaka vipaji vya kuigiza Katika Kanda ya Kati ambayo
inawakilishwa na Mkoa wa Dodoma. Shindano hili linaendelea ambapo awali
lilianzia Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza na hatimaye kupatikana kwa
washindi watatu wa kanda ya Ziwa huku wakisubiri washindi wa Kanda
nyingine kupatikana Kwaajili ya fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar
Es Salaam na mshindi mmoja kuibuka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za
Kitanzania.
Timu
nzima ya Proin Promotions Limited ambao ndio waratibu na waendeshaji wa
Shindano hili tayari wapo sawa kwa shughuli hiyo katika kanda ya kati.
Zoezi la kusaka Vipaji vya Kuigiza katika Kanda ya Kati itafanyika
Mkoani Dodoma ambapo litaanza tarehe 12 Aprili 2014 katika Ukumbi wa
African Dreamz uliopo Area C Mjini Dodoma.
Mpaka
Sasa kanda zilizobakia ni Kanda ya Juu Kusini ambapo Mkoa
utakaowakilisha ni Mbeya, Kanda ya Kusini usaili utafanyika Mkoani
Mtwara, Kanda Pwani usaili utafanyika Mkoa Dar Es Salaam na Kanda ya
Kaskazini usaili utafanyika katika Mkoa wa Arusha huku Mkoa wa Kigoma
ukipewa upendeleo wa kuiwakilisha Kanda ya Ziwa tena ambapo tayari zoezi
hilo ndipo lilipoanzia Mkoani Mwanza.
Kabla
ya Usaili wa kusaka Vipaji vya Kuigiza Kuanza Siku ya Ijumaa kutakuwa na
Promotion Party itakayofanyika Katika Ukumbi wa Disco wa 84 kuanzia saa
tatu usiku na kuendelea Wakazi
wa Kanda ya Kati wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya
kuonyesha Vipaji vyao na kuitumia fursa hii katika kukuza vipaji vyao
Comments