Twanga Pepeta kupamba utambulisho Miss Tabata SIKU YA Pasaka

 Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” itasindikiza uzinduzi wa Redds Miss Tabata itakayofanyika Jumapili ya Pasaka katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema bendi hiyo itatambulisha nyimbo zao mpya kama zawadi yao ya Pasaka kwa wapenzi wao.
Pia bendi hiyo ijulikanayo kama Wakali wa Kisigino pia watapiga nyimbo zao zote kali hadi majogoo.
Mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo hao siku hiyo kabla hawajashiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi ujao.
Katika uzinduzi huo warembo wa Tabata watasindikizwa na washiriki wenzao wa Miss Mzizima na Miss Ukonga.
Pia watakuwepo viongozi waandamizi kutoka kamati ya Miss Tanzania ikiongozwa na Hashim Lundenga na Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa.
Warembo 21 wanaendelea na mazoezi ya Miss Tabata katika ukumbi wa Da West Park chini ya wakufunzi wawili -  Neema Chaki na Pasilida Bandari.
Warembo hao ni Esther Frank Kiwambo (20), Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18), Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wengine ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21),  Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19) na Ramta Mkadara (20).
Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata ni  Dorice Mollel ambaye pia ni Redds Miss Ilala.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*