UFUNGUZI WA WARSHA YA KUJENGA UELEWA WA WADAU KUHUSU MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI – TASAF AWAMU YA TATU MKOANI KATAVI
Picha
hii na zingine zilizopo chini yake ni za picha ya pamoja ya Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe (wa tatu kwa waliokaa) na makundi
mbalimbali ya washiriki wa warsha ya kujenga
uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru Kaya maskini – TASAF awamu ya
tatu Mkoani Katavi, wengine waliokaa kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Mpanda Bw. Seleman Lukanga, Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Bw. Paza Mwamlima na Meneja uratibu TASAF Tunu Alice Munthali.
Wengine ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Enock Gwambasa na Makamu
M/Kiti Yusuf Msengi Ngassa.
Meneja
Uratibu kutoka TASAF Makao Makuu Tunu Munthali (aliyesimama)
akiwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe (wa kwanza
kulia) salaam za Mkurugenzi mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,
Dkt. Rajabu Rutengwe akihutubia washiriki wa Warsha ya kujenga uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kunusuru Kaya
maskini – TASAF awamu ya tatu Mkoani Katavi .
Hawa
nao ni sehemu ya washiriki wa warsha hiyo inayoshirikisha watendaji
mbalimbali wa ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa na Kata wakifuatilia kwa
makini maelezo ya ufunguzi toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab
Rutengwe (hayupo pichani)
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo
wakimsikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab
Rutengwe (hayupo pichani)
Comments