MUIMBAJI
wa Kimataifa raia wa Uingereza Ayobami David ni mmoja wa waimbaji
watakaoshiriki katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Aprili 20
katika mikoa nane hapa nchini. Ayobami ni muimbaji ambaye anafanya vizuri katika muziki huo wa Kumtukuza Mungu kupitia nyimbo mbalimbali.
Awali
Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka inayoongozwa na Mwenyekiti
wake, Alex Msama ilijipambanua kwamba tamasha la mwaka huu wanatoka
kivingine ili kuendana na kasi ya Sayansi na Teknolojia kwa
kuwashirikisha waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania. Kwa
mujibu wa Msama kwa kuwa wameamua kukuza muziki huo hapa nchini, dhana
hiyo itafanyika kila kona ya dunia ili Tanzania ipige hatua zaidi katika
tasnia ya muziki huo.
Msama
alisema miaka iliyopita walikuwa wakiwatumia katika matamasha yake
yaliyoasisiwa tangu mwaka 2000, waimbaji kutoka Kenya, Zambia, Afrika
Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kwingineko. “Niliyoeleza
mwanzoni yanakamilika, kwa sababu nilidhamiria kuliboresha zaidi
Tamasha la Pasaka kwa kuwashirikisha waimbaji wa Kimataifa, mashabiki
wakae mkao wa kula kupata ladha tofauti katika tamasha la mwaka huu,”
alisema Msama.
Aidha
Msama alisema mbali ya Ayobami, Kamati imemuongeza muimbaji wa injili
raia wa Rwanda, Lilliane Kabaganza ingawa bado taratibu zinaendelea
kuwapata waimbaji wengine wa kimataifa. Mbali
ya waimbaji hao wa Kimataifa, wengine ni Rebecca Malope, Keke Phoofolo
(Afrika Kusini), Ephraim Sekereti (Zambia), Faraja Ntaboba (DRC) na
Sarah K, Paul Mwai (Kenya).Baadhi
ya waimbaji wa Tanzania waliothibitishwa kushiriki katika tamasha hilo
ni pamoja na John Lisu, Rose Muhando, Upendo Nkone na Upendo Kilahiro.
Comments