Airtel Public Relations Manager Jackson Mbando speaks to the media at a
press conference to announce the forthcoming Manchester United International
Soccer Clinic to be held in Dar es Salaam from 23rd-27th
April under the tutelage of coaches from Manchester United Soccer Schools. He is flanked by the Tanzania Football
Federation (TFF) President Jamal Malinzi .The event was held at the Airtel
Tanzania Headquarters, 18th April 2014.
Tanzania Football Federation (TFF)
President Jamal Malinzi speaks to the media at a press conference to announce
the forthcoming Manchester United International Soccer Clinic to be held in Dar
es Salaam from 23rd-27th April under the tutelage of
coaches from Manchester United Soccer Schools.
He is flanked by Airtel Public Relations Manager Jackson Mbando.The event was held at the Airtel Tanzania
Headquarters, 18th April 2014.
======== ======= ========
Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars kutua Dar
Jumatatu
·
Ni
kutoka nchi 12 Afrika
·
Waziri Bernard Membe mgeni rasmi siku ya ufunguzi
·
Kliniki kuendeshwa na makocha kutoka Manchester United
Dar es Salaam, Ijumaa 18 Aprili, 2014. Wachezaji wa soka
chini ya umri wa miaka 17 kutoka nchi 12 barani Afrika wanatarajiwa kuwasili
jijini Dar es Salaam Jumatatu Aprili 21 kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa.
Hii ni mara ya pili Tanzania imepewa
heshima ya kuwa mwenyeji wa kliniki ya kimataifa baada ya ile iliyofanyika
kwenye uwanja wa wa kisasa wa Taifa mwaka 2011.
Kliniki
ya mwaka huu itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam, Chamazi, nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam inakutanisha wachezaji chipukizi, wasichana na wavulana,
kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville,
DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania. Mafunzo hayo ya siku tano mfululizo chini ya makocha wazoefu kutoka klabu
maarufu duniani ya Manchester United yana lengo la kuwapa vijana mbinu
mbalimbali za kisoka hasa katika eneo la ushambuliaji.
Kliniki hii ya kimataifa inashirikisha vijana waliofanya vizuri mwaka jana
katika mashindano ya Airtel Rising Stars kwenye nchi zao pamoja na washindi wa
mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini Nigeria ambapo timu ya wasichana
ya Tanzania ilitwaa uchampioni wa fainali hizo hizo.
Hafla ya uzinduzi wa kliniki hiyo imepangwa kufanyika siku ya Jumatano
kwenye uwanja wa Azam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa mgeni rasmi.
Membe anatarajiwa kuwahamasisha vijana kujituma ili kuweza kuendeleza
ipasavyo vipaji vyao vya soka.
Hafla hiyo ya uzinduzi pia inatarajiwa kuhudhuriwa na mabalozi kutoka nchi
zinazoshiriki kwenye kliniki hiyo itakayojumuisha mafunzo ya uwanjani na ya
darasani. Vipindi vyote hivyo vitafanyika pale pale Azam Complex.
Comments