ALIYEBWAGA KIMAPENZI NA DIAMOND BADO ATESEKA MOYONI, NI MTANGAZAJI WA KIKE KITUO CHA TV JIJINI DAR ES SALAAM.

http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/07/penny_7.jpg
MPENZI wa zamani wa msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’, anashukuru Mungu kwani tangu siku aliyobwagwa na mpenzi wake huyo, kaka zake walikuwa faraja kubwa wakimsihi awe na moyo mgumu wa kuikabili hali hiyo.

Mojawapo ya vitu ambavyo wamekuwa wakimtia moyo, Penny alisema ni kumwambia kuwa yeye ni mrembo na hakuna anayemfikia na kumtaka ajiamini kwa hilo.

Akizungumza katika kipindi cha Mkasi kinachorushwa na EATV, mrembo huyo ambaye ni mtangazaji wa kituo cha DTV, alisema tangu alipokuwa na mahusiano na Diamond, kaka zake walikuwa wakimtahadharisha, lakini kwa kuwa alikuwa bado hayajamfika, hakusikia la mtu.

Hata hivyo, alidai anashukuru hata hilo la kubwagwa lilipomkuta hawakumbeza na badala yake walikuwa naye pamoja na kuongeza kuwa yote inatokana na malezi ya upendo ambayo wamelelewa ndani ya familia yao tangu wakiwa wadogo.

Anakiri kuwa jambo lililomtokea linaweza kumpata mwingine pia, japokuwa yeye linaonekana kuongelewa sana kwa kuwa ni mtu maarufu.

Akimzungumzia Wema Sepetu, alisema hana ugomvi naye na kamwe hawezi kumchukia labda kama yeye ndio atafanya hivyo kwake.

Katika mahojiano na kipindi hicho, Penny wakati wote alionekana akijitahidi kupotezea maswali yanayomuhusu Diamond na watangazai kadiri walivyozidi kumbana alikuwa akiwajibu kwa kifupi.

Moja ya swali ambalo alionekana kujiumauma ni la pete ya uchumba aliyovaa, ambapo awali alisema amevalishwa na wakati mwingine akidai amejivika mwenyewe, jambo ambalo liliwaacha wengi njia panda wasijue ukweli ni upi.TANZANIA DAIMA.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA