BRAZIL NA UJERUMANI KUVAANA NUSU FAINALI, UFARANSA NA COLOMBIA ZATUPWA NJE
Matokeo hayo yanaifanya Ufaransa kuaga mashindano ya kombe la Dunia huku Ujerumani ikijiandaa kuvaana na wenyeji wa michuano hiyo, timu ya Taifa ya Brazil Julai 08 mwaka huu.
Mtanange mwingine uliopigwa hapo jana ni ule uliowakutanisha wenyeji Brazil walioipa kipigo cha bao 2 – 1 Timu ya Taifa ya Colombia katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Estadio Castelao na kushuhudiwa na marais wa mataifa yote mawili.
Mlinzi wa kati wa Brazil anayechezea klabu ya PSG ya Ujerumani, Thiago Silva aliweza kuiandikia timu yake bao la kuongoza mnamo dakika ya saba na kufuatiwa na David Luiz aliyeipatia Brazil bao la ushindi kabla ya Straika wa kutumainiwa wa Colombia, James Rodriguez kufunga bao moja kwa mkwaju wa penalti dakika ya 80′ ambalo halikuweza kugeuza matokeo hayo.
Comments