BREAKING NEWZ; MWIMBAJI MWINGINE WA MUZIKI WA INJILI NCHINI AFARIKI DUNIA


Zikiwa ni takribani wiki tatu tangu tasnia ya muziki wa injili nchini kumpoteza mmoja wa waimbaji wake marehemu mchungaji Debora Saidi, taarifa ambazo GK imezipata ni kwamba mwimbaji mwingine wa muziki wa injili Orida Njole amefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Orida ambaye mpaka umauti unamfika mchana wa leo ilikuwa bado haijajulikana nini hasa kinamsumbua lakini alikuwa ameishiwa damu sana, mpaka umauti unamkuta alikuwa anatamba na album yake iitwayo 'Duniani tu wapitaji' huku kwa mujibu wa watu waliomfahamu marehemu wameeleza kwamba alikuwa mtu mchangamfu wakati wote wakati wa uhai wake na kwamba wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe!

Picha ya mbele ya álbum ya marehemu Orida Njole.

Marehemu Orida akiwa na mtoto yatima katika kituo cha Tosamaganga Iringa alipotembelea kituoni hapo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA