Dk. Kashilillah awasihi Wabunge wanawake wa Afrika

Na Mwandishi Wetu, Arusha

WANAWAKE wa Bara za Afrika wametakiwa kujihusisha kikamilifu kwenye ushiriki wa shughuli za maamuzi ili waweze kufikia malengo ya maendeleo wanayoyakusudia..

Wito huo umetolewa jana na Katibu wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola wa Kanda ya Afrika (CPA) Dk. Thomas Kashilillah alipokuwa akizungumza katika kikao cha Kamati ya Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola wa Kanda ya Afrika, kilchokuwa kikijadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo ikiwemo uwezeshaji wa wanawake katika masuala ya uwakilishi.

Dk. Kashilillah ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema wakati umefika sasa kwa wanawake wa Bara la Afrika kujihusisha kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kikanda na kishiriki simian na makongamano mbavyo vitawajengea uwezo zaidi katika shughuli zao.

“Sasa ni wakati muafaka kwa wanawake kwa wanawake wa ukanda huu kujihusisha kikamilifu katika shughuli za maamuzi kwenye kanda yetu na kushirikia semina na makongamano mbalimbali ambayo yatawajengea uwezo zaidi katika shughuli zao.” Alisema Dk. Kashilillah.

Aliwataka wanawake kuangalia namna ambayo wanaweza kuanzisha jukwaa lao litakalowawezesha kujadiili mambo ambayo yana maslahi kwao ambalo linaweza kuwa linakutana mara mbili kwa mwaka ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea kimaendeleo.

Alisema, wanawake wanaweza kutumia nafasi ya mikutano ya mwaka ya CPA ambayo ni washiriki kukutana kabla ya kuanza kwa vikao vyake ambapo watapata nafasi ya kubadilishana mawazo na uzoedu katika mambo mbalimbali.

Naye mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo kutoka Bunge la Tanzania, Anna Abdallah, akichangia mjadala huo, alisema kupitia mipango ya aina hiyo ya uwezeshaji wanawake, Tanzania imeweza kupiga hatua kubwa ya kuwajengea akina mama uwezo wa kiuongozi na kuingia katika vyombo mbalimbali vya maamuzi.

Alisema hivi sasa Tanzania ni moja ya nchi zilizo na uwakilishi wa kutosha wa wanawake katika ngazi mbalimbali za uongozi na ushiriki katika nafasi walizo nazo umekuwa na manufaa na mafanikio makubwa.

Mwisho.

   




Spika Makinda akumbusha wajibu wa waandishi

Na Mwandishi Wetu, Arusha

WAANDISHI wa habari na vyombo vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kuandika habari za mambo ya kibunge vimetakiwa kufanya jitihada binafsi za kujifunza na kuelewa shughuli zinazofanywa na Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola ya Kanda Afrika (CPA) ili viwe na uwezo wa kuandika taarifa sahihi kulingana na matakwa ya kazi za kibunge.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Rais wa Umoja wa Mabunge wa Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Anna Makinda, ambaye ni mwenyeji wa mkutano wa 45 wa umoja huo unaofanyikia mkoani Arusha na kuhudhuriwa na zaidi ya wajumbe 500 kutoka nchi 18 za ukanda huu ambazo ni wanachama.

Spika Makinda alisema CPA imebaini kuwa waandishi na vyombo vya habari ni nguzo muhimu inayoweza kusaidia mipango na shughuli zinazofanywa na umoja huo.

Alisema CPA ni taasisi muhimu inayosaidia mabunge ya nchi wanachama na serikali zake katika Nyanja mbalimbali.

“Waandishi wa habari na vyombo vya habari kwa ujumla mnatakiwa kujikita kwa undani kuripoti shughuli zinazfanywa na CPA kama mtaielewa taasisi hii kwa undani. Nawaasa waandishi wa habari muwe na maslahi na taasisi hii kwa kuielewa vizuri ili muwe katika nafasi nzuri ya kuwa na mamlaka ya kuandika habari zake,” alisema Spika Makinda.

Alisema Bunge linatumia nafasi ya uwepo nafasi za kijifunza kupitia CPA  kutoa mafunzo ya aina mbalimbali kwa wabunge hivyo hata waandishi wa habari nao w anaweza kutumia mwanya huo kutafuta nafasi ya kupata mafunzo yanayohusu shughuli za kibunge.



Mwisho.

 Muundo wa CPA kanda ya Afrika kubadilishwa

Na Mwandishi Wetu, Arusha


RIPOTI ya mapendekezo ya mambo yanayopaswa kufanywa ili kuuwezesha Umoja wa Mabunge wa Jumuiya wa Madola Kanda ya Afrika (CPA) kuwa na mtizamo wa kimataifa zaidi inatarajiwa kuwasilisha katika mkutano mkuu wake wa 45 unaofanyika mjini Arusha.

Uamuzi wa kuwasilishwa kwa RIPOTI hiyo ulifikiwa jana na Kamati ya wawakilishi wa mabunge wanachama wa umoja huo iliyoketi katika ukumbi wa mikutano ilio kwenye hoteli ya kitalii ya Ngurdoto.

Akizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Seneta Letapata Makhaola wa Lesotho ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Katibu Mkuu wa CPA, Dk. Thomas Kashilillah, alisema ripoti hiyo inatokana na mapendekezo ambayo timu ya wataalamu wa kisheria walipewa na kutakiwa kuyafanyia utafiti wa kitaalamu ili waweze kutoa hali halisi inavyotakiwa kuwa katika mabadiliko yanayotarajiwa kufanyika.

Alisema ripoti hiyo itawasilushwa kabla ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano Julai 24 ili kutoa nafasi kwa wajumbe kuijadili na kutoa mapendekezo ya mabadiliko yanayotakiwa kufanywa ambayo yatasukuma kuandaliwa kwa Katiba mpya ya CPA.

“Ripoti hiyo itawasilishwa katika mkutano huu 45 na makubaliano yatakayofikiwa yatawasilishwa kwa maspika wa mabunge wa nchi wanachama ambao wataombwa kuyawasilishwa kwa wakuu wan chi mapendekezo ya mabadiliko,” alisema Dk. Kashilillah.

Umoja wa Mabunge wa Jumuiya za Madola Kanda ya Afrika umefikia hatua ya kutaka kufanya mabadiliko katika muudo wake wa sasa wa taasisi ya hiari iliyosajiliwa chini ya sheria za Uingereza.

Kwa miaka mingi, nchi wanachama wa CPA wamekuwa wakilalamikia muundo wa sasa wa taasisi hiyo kuwa wa hiari na kutaka kufanyika mabadiliko ya muundo wake jambo ambalo sasa linaelekea kutekelezwa.
 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA