FILIKUNJOMBE AILIPUA VODACOM KWA KUMDANGANYA RAIS

Mbunge  wa  Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe akililalamikia kampuni la simu za  viganjani Voda  Com katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Njombe leo  kuhusu  kudaiwa  kumdanganya Rais Jakaya Kikwete katika  uzinduzi wa mtambo wa 3G Njombe. (picjha na Francis Godwin)

Na Francis Godwin Njombe

MBUNGE  wa  jimbo la Ludewa  Deo  Filikunjombe ametaka serikali ya  mkoa  wa  Njombe kuuweka kitomoto uongozi wa kampuni ya simu za viganjani Voda Com kutokana na kudaiwa  kumganganya Rais Dr  Jakaya  Kikwete kuzindua mnala wa 3G ambao haufanyi kazi kwa  uwezo wa  3G.

Akizungumza  jana katika kikao  cha kamati ya  Ushauri mkoa (RCC) mkoa wa  Njombe mbunge  huyo alisema  kuwa iwapo  uongozi  wa  mkoa wa Njombe  utashindwa kuliweka kitimoto kampuni  hilo la Voda Com kwa  hatua  yake ya kudanganya  wananchi wa Njombe na kumdanganya  Rais kwa upande  wake atalifikisha suala  hilo  bungeni Dodoma.

Kwani  alisema  kuwa  kati  ya maeneo  ambayo mtandao  wa Voda  unasumbua katika upande wa Intarnet ni  pamoja na Njombe mjini ambapo mtandao  upo taratibu  zaidi  ukilinganisha na Ludewa ambako hakuna  huduma ya 3G.

Hivyo  aliwataka  wahusika wa mtandao  huo  kuangalia  uwezekano  wa  kusema ukweli badala ya  kudanganya na  kuwa kitendo  cha Rais kudanganywa ni aibu kwa  uongozi wa  mkoa mzima wa Njombe .

:"Nitakuwa  kiongozi wa  mwisho  katika  mkoa  wa Njombe kulifumbia macho suala hili la udanganyifu  lililofanywa na kampuni  hiyo ya Voda Com na iwapo mkoa utashindwa  kuwaita kwa  muda  unaotakiwa  basi  yeye kama mbunge atalifikisha suala  hilo bungeni ila bunge kutoa kauli "

Mbunge Filikunjombe  alisema  zipo  jitihada  mbali mbali  zinazofanywa na makampuni ya simu katika kusogeza  mawasiliano  vijijini kwa  wananchi  ila ni vizuri makampuni hayo  kueleza  ukweli kwa  wananchi  juu ya huduma za mawasiliano

Aidha  alisema kuwa  ni  vema Voda  Com  kufika  mjini Njombe na  kuangalia  tatizo  la wateja  wake  waliopo umbali  wa  mita  takribani 20 hadi 100 kukosa  huduma hiyo ya 3G ili  kulifanyia  marekebisho

Katika  hatua nyingine mbunge  huyo  aliitaka serikali ya  mkoa  wa Njombe kurejesha ada katika  shule za msingi kuliko  kuendelea  kuwasumbua  wazazi kwa  michango  isiyokwisha  ambayo ni kero  kubwa kwa  wananchi.

Alisema  kuwa iwapo  serikali inataka  kuboresha  elimu ni vizuri kuwe na utaratibu  mzuri wa  kuchangisha  michango kwa  wazazi kuliko kuwadanganya  wananchi  kuwa ada  imefutwa  huku michango ikiendelea  kuwa mingi kuliko hata ada.

Pia  alisema kama ada  imefutwa  basi mkoa  kuweka utaratibu mzuri wa michango ambayo itajulikana kwa  wananchi  wote  ili waweze  kujipanga
Mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.