JOSE MOURINHO KUMRUDISHA DARAJANI GWIJI WA CHELSEA DIDIER DROGBA

   
 

 


Legend: Mourinho (left) brought Drogba to the club in 2004 from Marseille, and his faith paid off
Gwiji: Mourinho (kushoto alimleta Drogba katika klabu ya Chelsea mwaka 2004 akitokea Marseille ya Ufaransa.

Imechapishwa Julai 10, 2014, saa 9:49 alasiri

KLABU ya Chelsea inaangalia uwezekano wa kumrudisha Didier Drogba katika dimba la Stamford Bridge.
Nyota huyo mwenye miaka 36 anazivutia klabu za Qatar, wakati Juventus nao wakifikiria kumnasa mkongwe huyo anayecheza katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki.
Bado Jose Mourinho ana mahusiano mazuri na Muivory coast huyo na anavutiwa kumrudisha kwa majukumu ya ukocha zaidi.
Elsewhere: The 36-year-old has interest from clubs in Qatar while Juventus continue to flirt with the idea
Mkongwe huyu wa miaka 36 anazivutia klabu za Qatar, nao Juventus wanaitaka saini yake.

Klabu hizo za Qatar zinatarajia kutoa ofa nono na mshahara utajadiliwa, lakini unakadiriwa kuwa paundi milioni 3 kwa msimu baada ya makato ya kodi.
Wazo la kurudi Chelsea litaangaliwa zaidi na pande zote.
Mourinho amekuwa na mapenzi makubwa kwa Drogba na anajua kuwa atakuwa na msaada mkubwa katika kikosi chake msimu ujao.
Alionesha nia hiyo hata Galatasaray ilipokutana na Chelsea katika michuano ya UEFA mwezi machi mwaka huu na alieleza kuwa Drogba anaweza kurudi na yuko makini kufanikisha hilo.
Drogba alishinda makombe matatu ya ligi, makombe manne ya FA na kombe la UEFA akiwa katika klabu ya Chelsea na Mourinho anataka kutumia uzoefu wake kuwashauri wachezaji wake wapya.
Return? Drogba was Chelsea's hero in the 2012 Champions League final win over Bayern Munich
Anarudi? Drogba alikuwa shujaa wa Chelsea mwaka 2013 waliposhinda dhidi ya Bayern Munich na kutwaa ndoo ya UEFA

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*